Wachunguliaji! Je kuna sababu ya wewe kuziba kamera ya kompyuta yako?

1
Sambaza

Je kuna sababu ya wewe kuziba kamera ya kompyuta yako, yaani webcam? Sababu ipo, mambo mengi yametokea ndani ya miaka kadhaa sasa yanayoonesha na kwa namna gani watu wanaweza kukuchunguza kwa kutumia webcam ya kompyuta yako.

Fahamu kuhusu Blackshades RAT

Tayari kuna juhudi nyingi za kimataifa zikiongozwa na vyombo vya usalama Marekani vinasaka na kuwachukulia hatua watumiaji wa programu hii

Blackshandes RAT ni programu inayomilikiwa na maelfu ya watumiaji na ni programu spesheli iliyotengenezwa kwa ajili ya kuwasaidia wadukuzi kuweza kuchunguza kompyuta za watu wengine walio maelfu ya kilomita kwa njia za mtandao. Wadukuzi wanaweza kuiba mafaili, kutumia kamera na mic ya kompyuta waliyofanikiwa kuidukua.

SOMA PIA:  Utaweza Kubackup Kompyuta Nzima kupitia Google Drive

Mmoja wa watu waliohusika na utengenezaji wa programu hiyo tayari ashachukuliwa hatua za kisheria mapema mwaka huu lakini hili halijazuia wengine wengi kuendelea kuitumia.

kuziba kamera ya kompyuta

Ata mwanzilishi wa mtandao maarufu wa Facebook katika picha hii watu waligundua amehakikisha anaziba eneo la kamera ya laptop yake na kwenye Mic pia.

Picha za uchi za Miss Teen USA

Kijana mmoja mdogo, Bwana Jared James Abrahams alikamatwa na kufunguliwa mashtaka baada ya kufanikiwa kupata picha za uchi za mshindi wa shindano la Miss Teen USA huko Marekani. Na alitumia programu ya Blackshades RAT kufanikisha udukuzi wake.

  • Alimtumia binti huyo barua pepe iliyomrubuni kupakua programu ya Blackshades RAT bila kufahamu.
  • Moja kwa moja kijana huyo aliweza kupata uwezo wa kuona mambo yote moja kwa moja kupitia webcam ya mdada huyo kwa miezi na miezi. Hili lilimuwezesha kumpiga picha za uchi binti huyo pale alipokuwa mwenyewe chumbani n.k,.
  • Tayari watu wengi washakamtwa nchini Marekani na barani Ulaya kwa matumizi ya programu hii.

Muonekano wa ndani ya programu hiyo, hapa mdukuzi anamuangalia binti asiyefahamu ya kwamba anatazamwa kupitia kamera yake ya kompyuta – webcam

Pia kuna suala la wadukuzi wa kiserikali – kama vile NSA/CIA

Pia kuna wanaofanya uamuzi wa kuziba eneo la Webcam kutokana na kutaka kuepuka udukuzi unaofanywa na vyombo vya kijasusi vya kimataifa kama vile CIA. Katika data zilizowekwa wazi na mmoja wa watu waliokwisha fanya kazi na mashirika kama NSA/CIA, Bwana Snowden alisema mashirika hayo yanateknolojia kubwa zinazowezesha kudukua kwa urahisi vitu kama kompyuta au simu za mamilioni ya watu duniani.

SOMA PIA:  BarraCuda Pro: Diski uhifadhi ya ukubwa wa TB 12 kwa ajili ya kompyuta za mezani

Fahamu mara nyingi watumiaji wa Blackshades RAT baada ya kufanikiwa kupata picha za uchi za mtu basi uanzisha utapeli wa kutishia kuziweka wazi mitandaoni kama mtu hatatuma zingine au ata pia kama hawatapokea malipo flani.

Vipi una mtazamo gani juu ya udukuzi wa aina hii? Unataka kuwa salama zaidi??? hakikisha umefunika kamera ya kompyuta yako…usijisikie huru sana na kujiachia ukiwa na kompyuta yenye webcam mbele yako.

Kumbuka kusambaza makala na pia kuungana nasi kupitia Facebook, Twitter, Instagram, YouTubeTelegram na Google Plus

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com