Wadukuzi wa OurMine wadukua akaunti za Twitter. - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Wadukuzi wa OurMine wadukua akaunti za Twitter.

0
Sambaza

OurMine sio jina geni kwa mashabiki wa usalama wa katika mitandao, ni kundi la wadukuzi wasio na lengo baya bali kusaidia kuonesha udhaifu wa mitandao (hii ni kwa mujibu wa kundi hilo).

see url

Kundi hili limeingia katika mitandao ya habari baada ya kuzidukua akaunti kadhaa katika mtandao wa Twitter, akaunti za Netflix, Marvel na NFL zimekumbwa na kasheshe hilo siku kadhaa zilizopita.

go to link

http://thd-industries.com/category/uncategorized/ OurMine walichukua umiriki wa akaunti za Twitter za Netflix US, Black Panther, Captain America, Iron Man, Ant-Man, Thor na Doctor Strange lakini pia kwa mujibu wa taarifa kutoka katika mtandao wa IBTimes kundi hilo liliweza kuchukua umiliki wa akaunti ya ligi ya taifa ya mpira wa miguu ya marekani (NFL).

INAYOHUSIANA  Google ina kifaa chake cha kudhibiti udukuzi

OurMine wanasisitiza kwamba wao wanafanya hivi sio kwa lengo baya bali kwaajiri ya kuyaonesha makampuni hayo kwamba usalama wao ni mdogo, wadukuzi hawa huchukua umiliki wa akaunti na kuweka ujumbe kujitambulisha na kutoa ofa ya kusaidia kuboresha usalama wa akaunti hiyo.

ourmine

Screenshot ya ukurasa wa Twitter wa Marvel baada ya kudukuliwa.

Wadukuzi hao pia ndio wale wale walioweza kudukua akaunti ya Twitter ya Jack Dorsey ambaye ndiye Mkurugenzi Mtendaji wa Twitter pamoja na akaunti ya Twitter ya Sundar Pichai ambaye ni Mkurgenzi mtendaji wa Google. Hivyo kama ulikuwa unalichukulia powa kundi hili jua wazi ni watu ambao wanauwezo mkubwa saana.

INAYOHUSIANA  Kodi kwenye mitandao ya kijamii yaanza rasmi Uganda

Tayari akaunti zote zilizodukuliwa zimerudishwa katika umiliki wa wahusika na tayari wamekwisha futa Twiti zote ambazo kundi hilo lilizichapisha.

Kumbuka kusambaza makala na pia kuungana nasi kupitia Facebook, Twitter, Instagram, YouTubeTelegram na Google Plus

Facebook Comments

Sambaza
Share.

Comments are closed.