Milioni 7 wakosa huduma za simu baada ya shambulizi la kimtandao Venezuela

Milioni 7 wakosa huduma za simu baada ya shambulizi la kimtandao Venezuela

0
Sambaza

Serikali ya nchi ya venezuela Alhamisi imesema kuwa shambulizi kubwa la kimtandao (Cyberattack) lililotokea mapema wiki hii limeathiri watumiaji simu za mkononi milioni saba kwa kukosa huduma.

Kikundi kinachojiita The Binary Guardians kimedai kuhusika na shambulio hilo la kimtandao kwa kusema shambulizi hilo lililenga Tovuti za serikali, mahakama, Tume ya uchaguzi na Bunge la nchi hiyo.

Divalproex buy fast “Nia yetu ni kutoa tumaini kwa watu bila kujali nguvu ya adui inayoonekana, kwamba kuna nguvu katika umoja,” ilinukuliwa barua pepe kutoka katika kikundi hicho juu ya shambulizi la kimtandao Venezuela.

shambulizi la kimtandao Venezuela

http://welovethegirls.com/motivational-monday-michelle-obama/ Shambulizi la kimtandao Venezuela: Muonekano wa moja ya tovuti za serikali baada ya kudukuliwa

where to buy flagyl for bv Shambulizi hilo ambalo liliharibu takribani Tovuti 40 za serikali, limedaiwa kufanywa na Kikundi hicho kuonesha hasira kwa kile kinachodaiwa kupinga ‘udikteta’ wa Rais Nicolas Maduro wa nchi hiyo.

INAYOHUSIANA  Kodi ya mitandao: Kampuni za simu kuzuia VPN nchini Uganda

Katika tovuti za serikali zilizodukuliwa zilionesha maneno yaliyosema ‘Operesheni David’ na Kipande cha picha kutoka filamu ya The Great Dictactor ya Charlie Chaplin.

“Hivi ni vitendo vya kigaidi vilivyoathiri kampuni ya Movilnet jumatano na kuacha mikoa saba bila ya mawasiliano na watu milioni saba kukosa huduma”, alisema Waziri wa Sayansi na Teknolojia Hugbel Roa.

Venezuela ina makampuni mawili binafsi yanayotoa huduma za mawasiliano nchini humo ambayo ni Digitel na kampuni ya inayomilikiwa na Spain ya Movistar.

Wazir Roa alisema mashambulizi hayo yalianza Jumatatu ambapo Tovuti kadhaa za serikali na makampuni binafsi zilidukuliwa.

Kwa msaada wa wataalamu kutoka nje ya nchi wamesaidia kurudisha huduma za kimtandao na mwasiliano katika hali ya kawaida. Alisema uchunguzi unaendelea Kubaini na kuwakamata waliohusika na shambulizi hilo.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.