Wakuu Wa Huawei Washikiliwa Na Polisi Kwa Tuhuma Za Kuvujisha Siri! - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Wakuu Wa Huawei Washikiliwa Na Polisi Kwa Tuhuma Za Kuvujisha Siri!

2
Sambaza

Wakuu wa kampuni ya Huawei wanashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kuvujisha siri za kampuni kwa kampuni linguine la teknolojia la huko nchini china, LeEco.

http://jaaci.org/2016/01/

Wakuu walioshoikiliwa na pamoja na wale wanaohusika na mambo ya kudizaini (design) katika uzalishaji. Pia taarifa zinigine zinasema kuwa wakuu hawa walikua sio waajiriwa wa Huawei wakati wanashikiliwa.

Huawei

Mpaka sasa taarifa ambaozo zimevuja kwa LeEco bado hazijawekwa wazi kwa sababu za kiusalama zaidi.

follow Huawei Na LeEco Kwa Ufupi.

LeEco ilianzishwa na Bw. Jia Yueting na ni kampuni la kichina ambalo mara nyingi linashughulika na teknolojia za magari, baiskeli za umeme, simu, VR (virtual reality), Tv na kuandaa filamu.

INAYOHUSIANA  Huawei na simu ya kwanza yenye RAM GB 8

Tangia mwaka 2016 kampuni ya LeEco imekua ikijitahidi sana katika kuhakikisha kuwa inatia maguu katika soko la U.S. kwa kuuza simu kwa bei ambayo watu wengi wanaweza kuimudu.

Kwa upande mwingine kampuni ya Huawei ilianzishwa mwaka 1987 na Bw. Ren Zhengfei na mpaka sasa ndio kampuni ya tatu kwa ukubwa duniani katika uzalishaji wa simu janja.

Kampuni hii makao makuu yake yapo huko Shenzhen, China na ina mafanikio makubwa ukilinganisha na kampuni ya LeEco

Hali hii ilivyotokea wachambuzi wengi wa Teknolojia walidai kuwa China ndio nchi pekee ambayo inaongoza kwa kuwa na ushindani katika soko la simu janja duniani kwa kuwa kuna wauzaji wengi wanapigania soko ili kuhakikisha kuwa wanabaki namba moja.

LeEco

http://freelineinc.com/about/ Mashtaka

INAYOHUSIANA  Huawei waendelea kutoa toleo jingine la simu za Honor

Ripoti zinasema kuwa wakuu hao 6 ambao wanashikiliwa walikua wanaweka wazi siri za uuzaji kwa ujumla kwa kampuni ya Coolpad Group ambalo asikimia kubwa ya hisa zake zinamilikiwa na kampuni ya LeEco.

Na pia iliripotiwa kuwa wakuu wawili kutoka katika kampuni ya Huawei walitoka katika kampuni hiyo na kujiunga na makampuni mengine. Kampuni ya LeEco imekana na kusema kuwa haikushiriki katika machakato huo wa kupokea siri za Huawei.

Kwa kuwa kampuni ya Huawei inafanya vizuri hivi sana ndio maana makampuni mengine yanachukua wakuu wa kampuni hiyo kwa kuwaahidi mishahara minono.

Mwaka 2016 huawei iliuza simu milioni 139 nje ya nchi (china) kulingana na taarifa kutoka Interntional Data Corp (IDC).

INAYOHUSIANA  VLC haipatikani kwa baadhi ya simu za Huawei

Raisi wa awali wa Huawei Bw, Liu Jiangfeng alijiunga na Coolpad Group mwezi agosti 2012, Na pia Xu Xinquan ambae alikua raisi wa biashara ya Huawei ya kwenye mtandao (e-commerce) nae aliiaga kampuni na kwenda kujiunga na kampuni ya LeEco vile vile.

Ningependa kusika kutoka kwako, wanasema mti wenye matunada hauachi kupigwa mawe, Je unaona hivyo kwa Huawei? Niandikie hapo chini sehemu ya comment.

Kumbuka kusambaza makala na pia kuungana nasi kupitia Facebook, Twitter, Instagram, YouTubeTelegram na Google Plus

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa Teknokona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com