Wamiliki Wa Facebook, Waja Na Mpango Kabambe Wa Kuzuia/Kutibu Magonjwa! - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Wamiliki Wa Facebook, Waja Na Mpango Kabambe Wa Kuzuia/Kutibu Magonjwa!

0
Sambaza

Mmiliki wa Facebook, Mark Zuckerberg kwa kushirikiana na mkewe (Priscilla Chan) wameanzisha mpango kabambe ambao una lengo kubwa la kutibu magonjwa.

buy generic augmentin online
Mpango huu unaitwa ‘Chan Zuckerberg Initiative’ ambapo ndani ya mpango huu Mke wa Mark amesema kuwa atatumia dola bilioni 3 za kimarekani ndani ya miaka kumi na hii ikiwa ni moja kati ya hatua zake za kusaidia kutibu magonjwa ya binadamu.

generic Lamotrigine online no prescription Kwa sasa mpango huo (Chan Zuckerberg Initiative) unawekeza dola milioni 6 za kimarekani katika mradi unaojulikana kama Biohub. Biohub ni kitengo cha uchunguzi kinachojitegemea na kipo katika chuo kikuu cha California huko San Fransisco.

buy generic Depakote Kitengo hicho kimejikita katika kutengeneza na kugundua vifaa vipya ambavyo kwa namna moja au nyingine vitasadia au vitatumika katika kutibu magonjwa.

BioHub

BioHub

Chan kwa hisia alisema kuwa kwa kipindi cha miaka miwili iliyopita yeye na mumuwe walikuwa wakiongea sana na wanasayansi, ukaichana na wale wenye majina makubwa na tuzo kadhaa pia waliongea hata na wale waliohitimu vyuoni.

INAYOHUSIANA  Mechi za La Liga kuonyeshwa bure na Facebook

Priscilla Chan anaamini maisha mazuri kwa watoto (kizazi kijacho) yanawezekana na wao (kizazi cha sasa) ndio kina jukumu la kuhakikisha kuwa wanakitengenezea mazingira mazuri kile kijacho na hii ikiwemo na kuwasaidia katika kutatua au kupata tiba za magonjwa kadhaa.

Lakini Priscilla Chan alisema kuwa hii haimaanishi kuwa hakuna mtu atakaye umwa bali kwa ana imaani watoto wetu na watoto wa watoto wetu wataumwa kwa kiasi kidogo sana. Na pia uwezo wa kugundua magonjwa na kuyatibu kwa uharaka utaongezeka.

zuckerberg
Baada ya Priscilla Chan kuongea ndipo ilipofika zamu ya Mark Zuckerberg, yeye kwa upande wake alisema kuwa kwa sasa plani yao kubwa ni kufuta au kuteketeza magonjwa ya moyo, maambukizi, kansa na magonjwa ya ubongo kwani kwa sasa ndiyo ambayo yanaongoza kuleta vifo duniani.

INAYOHUSIANA  Facebook: Kuwa na mafariki wengi zaidi ya kikomo

Mark anaamini kabisa kuwa hili linawezekana lakini cha msingi ni kwamba watu inabidi wawe na subira pia wawe wavumilivu wakati wao wanafanya machakato mzima.


Mpango huu uliaanzishwa kwa mara ya kwanza mwezi septemba mwaka jana (2015) na Mark na mkewe Chan na bado unaendelea mpaka sasa

chan-zuckerbergNingependa kusikia kutoka kwako niambie hii umeipokeaje hapo chini sehemu ya comment. Inapendeza sana kuona matajiri wanatujali sio?

Kumbuka kutembelea kona ya teknolojia Tanzania kila siku kwani TeknoKona Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa Teknokona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comments are closed.