´╗┐ Wanafunzi wa nchini China na Teknolojia katika Kuibia Mitihani

Wanafunzi wa nchini China Wapo Juu Kutumia Teknolojia ktk Kuibia Mitihani

1
Sambaza

Katika kufanya nini? Ndiyo, kama kichwa cha habari kinavyosema, wakati huku kwetu bado wanafunzi wanaendeleza njia za kizamani na kubuni mpya za kuibia majibu au kufanya udanganyifu wakati wa mtihani, wanafunzi wa nchini China ndio wanaongoza katika matumizi ya teknolojia ya kisasa katika kufanya udanganyifu huo.

follow link

http://cagancaglar.com/2011/01/15/tedxresette-kayitlar-icin-son-haftaya-girildi/ Kila kipindi cha mitihani walimu na hata baadhi ya shule zinatumia polisi katika kuhaha na kusaidia katika kugundua njia zitumiwazo na wanafunzi hao. Inasemakana ugumu wa mitihani yao pamoja na kuwa na mfumo unafanana wa nchi kama Tanzania wa kwamba mtihani wa mwisho kubeba miaka yote ya mtu aliyotumia shuleni unachangia katika kukuza tabia hii.

Mwanafunzi akikaguliwa kabla ya kuingia eneo la kufanyia mtihani

Kali zaidi imetokea hivi karibuni baada ya kugundulika ya kuwa vijana wameendelea zaidi kiteknolojia katika kuhakikisha wanafanikiwa katika kuibia kwa kutengeneza miwani ambayo inarekodi na kutuma picha hizo kwa mwingine. Hii ni katika mtihani maarufu zaidi ujulikanao kwa jina la Gaokao ambao unaweza kuufananisha na ule wa kuhitimu kidato cha sita kwa hapa bongo. Ukaguzi wa wanafunzi kuingia eneo la kufanya mitihani katika gaokao imebidi nao uwe wa kiteknolojia ya juu, na hivyo imekuwa kama vile mwanafunzi anapita uwanja wa ndege.

kuibia mitihani

Afisa Usalama akionesha Miwani aliyokamatwa nayo mwanafunzi

source Hivi kijana wa kibongo akipata vifaa hivi si atafaulu mitihani yote hapa bongo, au wewe unaonaje?

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Downloading vs Streaming : Fahamu Tofauti Kuu, Kipi bora zaidi?
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

1 Comment

  1. Pingback: Algeria yazuia mitandao ya kijamii kuzuia wizi wa mitihani

Leave A Reply