Wapenzi 20 na iPhone 7 ishirini vyawezesha Mchina kununua nyumba

0
Sambaza

Pale ambapo tunapoamua kuwa na mpenzi kingine cha kujiuliza ni “Je, tupo wangapi?” kwani baada ya kukuhabarisha utakubaliana na mimi kuwa hilo swali lina umuhimu mkubwa na wa kipekee sana katika mahusiano na yule umpendaye.

Suala la mtu kuweza kununua nyumba ni kama ndoto kwani Uchina bei za nyumba nchini humo zipo juu na hazitegei kushuka bali zinazidi kupanda bei kila siku.

Wazazi wake wanazeeka na yeye ndio binti mkubwa kwahiyo si vibaya akawa na nyumba yake ili aweze kuwasaidia vilivyo hapo baadae wakati uwezo wao wa kuyamudu maisha umekwisha.

SOMA PIA:  Simu ya LG G6: LG waonesha bado wapo makini na biashara ya simu

Ni pale aliwatumia wapenzi wake ishirini kila mmoja kwa wakati wake alimnunulia simu janja aina ya iPhone 7 ambayo alikuwa ameomba anunuliwe na kisha kuziuza simu hizo katika duka ambalo linanunua simu zilizokwisha kutumika. Simu zote aliziuza na kulipwa zaidi ya Tsh. 39.5m ambazo alizitumia kama kianzio cha ununuzi wa nyumba iliyo nje kidogo ya Uchina.

iPhone 7 ni simu ambayo imetokea kupendwa na wengi duniani lakini ni ghali.

iPhone 7 ni simu ambayo imetokea kupendwa na wengi duniani lakini ni ghali.

Kila simu moja aliiuza kwa dola za Kimarekani 898 ambazo ni sawa na zaidi Tsh. 1,975,600. iPhone 7 ilitoka na kuanza kuuzwa mwezi wa 9 mwaka huu.

Yawezekana likawa ni jambo la kushangaza na hata baadhi ya wasichana kushindwa kuwa na mpenzi hata mmoja na kujiuliza kuwa aliwezaje kuwa na wapenzi wote 20?! Wamediriki kumwomba kupitia vyombo vya habari aweze kuwapa mbinu lakini amekataa kuzungumzia suala hilo na kuomba jambo hilo lisiendelee kuzungumziwa tena.

SOMA PIA:  Samsung kuuza simu za Galaxy Note 7 tena, kwa bei nafuu!

Ni vigumu kujua kama mpenzi/wapenzi tulionao ni wa ukweli au vinginevyo ila TeknoKona inaona tusishawishike kirahisi kwa sababu tu amekuomba umtimizie jambo fulani. Wewe je, una una maoni gani?

Chanzo: BBC

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com