Wasimamizi wa makundi Whatsapp kukiona cha moto India

0
Sambaza

Kuwa msimamizi wa kundi katika whatsApp (WhatsApp Group Chat Admins) kwa wengi sio kitu kikubwa sana. Kimsingi ni kuwezesha kuongeza wanachama katika Kundi au kumuondoa yeyote katika kundi husika.

Hata hivyo nchini India ni zaidi ya hivyo, kuwa msimamizi wa kundi huko ni jambo linalomtaka msimamizi kuwa makini zaidi.

Kwa mujibu wa taarifa ya Economic Times serikali ya India na mahakama inataka kuwafanya wasimamizi wa makundi ya WhatsApp kuwa wasimamizi ambao watadhibiti taarifa za uongo zinazoenezwa na watu wengi kupitia whatsApp.

SOMA PIA:  Instagram Inaifanyia Majaribio InstaLive Kwenda Katika 'Screen' Inayogawanyika!

Kwa mujibu wa sheria mpya Msimamizi wa kundi anaweza kutupwa gerezani kama muhusika wa kusambaza habari za uongo endapo kama hakuchukua hatua ya kumtoa katika kundi lake na kumripoti Polisi.

whatsapp
Kama itatokea mtu ametoa habari ya uzushi katika Kundi basi msimamizi anatakiwa kumtoa (removed) katika kundi na kumripoti haraka zaidi Polisi ili hatua dhidi yake zifuate.

Kama habari ya uongo itazidi kuenea kwa kusambazwa kutokea kundi husika na msimamizi wa kundi hakufuata hatua hizo basi atachukuliwa hatua za kisheria kama aliyesaidia kupotosha umma.

SOMA PIA:  Udukuzi kwenye Instagram; Akaunti za watu maarufu zaingiliwa!

Lengo la hatua hii ni kusaidia kukabiliana na kuenea kwa taarifa za uongo. Nchini India watu zaidi ya milioni 200 wamejisaJIli katika WhatsApp.

Wakati wa kampeni za uchaguzi wa Marekani kulikuwa na taarifa nyingi za uongo na uzushi kupitia makundi ya whatsapp.

Na hata hivi karibuni pia iliripotiwa kwamba Ufaransa ilikuwa na mafuriko ya habari za uongo zilizokuwa zinapikwa kutokea makundi ya WhatsApp katika kampeni za uchaguzi unaopigiwa kura leo.

SOMA PIA:  Piga Selfie Na Itumie Kama Emoji Na App Ya Allo!

Facebook nao wameanza mpango wa kupambana na taarifa za uongo kupitia mtandao wao.

Kwa sasa Dunia imekumbwa na wimbi la taarifa za uongo na uzushi kupitia mitandao ya kijamii. Kuanzia taarifa mpaka picha nyingi zimekuwa za uongo na uzushi.

Kwanini watumiaji wa mitandao ya kijamii wamekuwa wako mbele katika kuzusha na kusambaza habari za uongo? tatizo ni nini au msukumo wao ni upi? Tupe maoni yako.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com