‘Wasiojulikana’ waiba simu za iPhone X zenye thamani ya 826 milioni

0
Sambaza

Wezi watatu wameiba Simu mpya za iPhone X baada ya kuvunja gari maalumu la kubebea mizigo la kampuni ya UPS lililokuwa limehifadhi simu hizo nje ya duka la Apple huko San Francisco nchini Marekani.

Tukio hilo la wizi lilitokea asubuhi ya siku ya Jumatano; inaelezwa watu watu waliokuwa wanaendesha gari nyeupe aina ya Dodge van walipita karibu na gari la UPS lilokuwa linajiandaa kushusha mzigo katika Stonestown Galleria shopping mall huko San Fransisco, ndipo ulipovunjwa mlango na kuondoka na furushi lililokuwa na simu hizo.

Taarifa ya polisi inasema wezi hao waliiba simu zaidi ya 300 zenye thamani  ya dola za kimarekani 370,000 sawa na Tsh 826,580,000.

Tukio hilo linaloonekana kama la kupangwa wafanyakazi wa Apple na UPS wanaisaidia polisi katika upelelezi wake wa kuwapata wezi hao. Mpaka sasa watu hao wajajulikana wala kukamatwa. Taarifa zinasema simu hizo zilizoibwa zinaweza zisiweze kutumika ndani ya Marekani kwani namba zake za IMEI zimehifadhiwa na ni rahisi kuzifunga.

SOMA PIA:  AppStore: Apple yaondoa VPN kwa simu za iPhone nchini China

Apple wamekuwa na kawaida ya kuuza simu zao katika maduka yao maalumu ili kupata fursa ya kuonana uso kwa uso na wateja wao na kupata kuwasikia maoni yao au ushauri wao. Simu za iPhone X zilianza kuuzwa Novemba 3 katika maduka yote ya Apple katika nchi za Marekani, Uchina na Uingereza.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com