Wastani wa watumiaji kwa siku: Snapchat Yaipita Twitter kwa mara ya kwanza

1
Sambaza

Miaka miwili iliyopita kama ungeniuliza kama Snapchat itakuwa maarufu kwa kiasi hichi nisingekuwa na uhakika, ila tayari app hii inakua kwa kasi siku hadi siku…na sasa imefikisha takribani wastani wa watumiaji milioni 150 kwa siku.

Data zinaonesha mtandao wa kijamii wa Twitter una wastani wa watumiaji milioni 140 kwa siku na hivyo hii inaonesha tayari Snapchat imeshaiacha nyuma Twitter.

Data za wastani wa watumiaji wa app hiyo kwa siku imevujishwa na mmoja wa wafanyakazi wa mtandao huo wa kijamii kwenda kwa mtandao/gazeti la habari la Bloomberg.

SOMA PIA:  Microsoft Translator app yaongezwa lugha nyingine ya kutafsiri

snapchat vs Twitter

Kupata picha tuu ya kwa kiasi gani ukuaji huu ni wa kasi sana kumbuka;

airtel tanzania bando

  • Mwezi Disemba 2015 Snapchat ilikuwa na wastani wa watumiaji milioni 110 kwa mwezi – hivyo katika miezi mitano wameweza ongeza zaidi ya watumiaji milioni 50 kwa siku.
  • Twitter ina miaka 10 wakati Snapchat ina takribani miaka 5 tuu

Pia data zinaonesha Snapchat itaendelea kukua kwa kasi zaidi ukilinganisha na Twitter ambayo ukuaji wake umekuwa mwendo wa kobe kwa miezi mingi sasa.

SOMA PIA:  Snapchat yajiandikisha katika soko la hisa! #Apps

Je unatumia app ya Snapchat? Unapendelea nini zaidi? Tu-add kwa jina letu TeknoKona

Soma makala mengine za Snapchat -> Teknokona/Snapchat

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com