Watafiti: Factory Reset katika Simu za Android Haifuti Data Zako Zote

0
Sambaza

Unafikiria kuuza simu yako hivi karibuni? Habari mbaya imetolewa na kundi la watafiti, limegundua ya kwamba kuna uwezekano mkubwa wa data za mtumiaji wa simu ya Android kuopolewa upya hata baada ya mtumiaji kufuta data zake kwenye simu kwa kutumia ‘Factory Reset’.

Programu endeshaji ya Android ndiyo maarufu zaidi katika eneo la simu na inakisiwa ya kwamba kati ya simu milioni 500 hadi 600 zinazotumika kwa sasa zinaweza kuibiwa data hata baada ya kufanyiwa Factory Reset. Katika utafiti wao walitumia simu 21 kutoka makampuni 5 makubwa ya simu za Android. Hata baada ya simu hizo kufanyiwa ‘Factory Reset’ walifanikiwa kuopoa data mbalimbali zilizokuwa zimehifadhiwa katika simu hizo.

Data ni nini?

Data ni mafaili ya aina yeyote unayohifadhi katika kifaa cha elektroniki. Mfano ni kama vile picha, nyimbo, namba za simu, barua pepe na taarifa mbalimbali kuhusu utumiaji wako wa apps ktk simu husika.

Reset android phone using factory data reset

Chaguo la ‘Factory Reset’

Simu zilizotumika katika utafiti huo zilikuwa zinatumia toleo la Android kuanzia Android 2.3 hadi 4.3. Asilimia 80% ya simu zilizotumika katika utafiti huo ziliweza kuibiwa data baada ya kufanyiwa ‘Factory Reset’, na njia ya kuzipata ni njia inayoweza kutumiwa na watu wowote wenye uwezo mkubwa na ujuzi (utundu) kwenye programu endeshaji ya Android.

SOMA PIA:  Firefox Send: Mozilla waja na huduma ya kutuma mafaili kwa usiri

Watafiti hao wamesema sababu kubwa ya hali hii inaweza ikawa inasababishwa na vifuatavyo;

  • Mapungufu/uzaifu wa teknolojia ya diski uhifadhi za teknolojia ya ‘Flash’ (flash disks) zinazotumika katika simuza siku hizi
  • Watengenezaji wa simu hizi kutoambatanisha na ‘drivers’ muhimu zinazoitajika na simu hizo kipindi cha ufutaji wa data kupitia ‘Factory Reset’.

Haijafahamika kama Google na makampuni mengine ambayo simu zao zilitumika katika utafiti huu wanachukua hatua yeyote kuhusu udhaifu huu, ila kwa kiasi kikubwa ni ugunduzi muhimu na utakaowalazimisha kufikiria upya kuhusu suala hili la usalama wa data za watumiaji wa bidhaa zao.

Soma Pia –Njia 3 Za Ku ‘Reset’ Simu Ya Android!

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Leave A Reply

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com