Wateja wa mtandao wa Smile: Majanga ya huduma na tetesi za kufunga kampuni - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Wateja wa mtandao wa Smile: Majanga ya huduma na tetesi za kufunga kampuni

0
Sambaza

Kwa takribani siku mbili hali imekuwa mbaya kwa wateja wa mtandao wa Smile walio katika baadhi ya maeneo hasa hasa ya jijini Dar es Salaam baada ya huduma kusua sua na ata kwa baadhi kukosekana kabisa.

go

Mtandao wa Smile Communications unamilikiwa na kampuni ya Smile Telecoms Holdings ya nchini Afrika Kusini.

purchase motilium online Vyanzo mbalimbali vinaonesha tayari kuna dalili ya kampuni hiyo kuuza biashara zake kwa Tanzania na hivyo kuondoka kabisa. Katika kipindi cha takribani mwaka mtandao huo umejikuta kwenye ushindani mkali kutoka kwa mitandao mingine inayotoa huduma za intaneti za 4G.

mtandao wa smile

i need to buy Depakote Wakati mtandao wa Smile unaanza ulikuwa unatoa huduma ya kasi sana, ila kwa sasa mitandao mingine pia imewekeza vizuri kwenye miundombinu yake na hivyo kuongeza ushindani @Picha na mtandao

Mtandao kama wa Smart umeweza kuwaibia wateja wengi wa kiofisi waliokuwa wanategemea Smile kwa kigezo cha bei nafuu, pia mitandao mingine ya simu kama vile Vodacom, Halotel na mingine imezidi kutoa huduma za kasi zaidi za intaneti za kuweza kushindana na za Smile, pia kumbuka mara nyingi vifurushi vya mitandao hii ni bei nafuu zaidi na pia ni rahisi mtumiaji kuhama katika mitandao hii kwa matumizi mengi kama vile kupiga na kupokea simu wakati kwa mtandao wa Smile kikuu ni intaneti tuu.

INAYOHUSIANA  Waliopewa dhamana ya kusimamia mifumo ya TEHAMA serikalini waonywa na kutakiwa kuzingatia weledi kazini

Mtandao wa habari za kibiashara wa The Exchange Tanzania umeripoti kushuhudia ofisi kadhaa zilizo maeneo mjini kufungwa na pia wateja wengi wa mtandao huo kuendelea kutopata huduma wakati vifurushi vimelipiwa na visipotumiwa vinafikia muda wake na hivyo wateja kupata hasara.

Tulijaribu kuuliza hali ya huduma na kama kuna taarifa rasmi juu ya hali hiyo kupitia mtandao wa Twitter, Smile hawakuwa na taarifa zaidi juu ya tatizo lao.

Wateja wa mtandao wa Smile: Majanga ya huduma na tetesi za kufunga kampuni

Wateja wa mtandao wa Smile na shida ya huduma. Mazungumzo kupitia mtandao wa Twitter.

Je wewe ni mtumiaji wa mtandao huu kwa huduma za intaneti? Tuambie umeathirikaje?

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.