Watumiaji intaneti kupitia simu wawazidi wanaotumia kompyuta!

Kwa mara ya kwanza; Watumiaji intaneti kupitia simu wawazidi wanaotumia kompyuta!

0
Sambaza

Watu wengi zaidi wanatumia huduma ya intaneti kupitia simu na tableti zao kuliko wanaotumia kompyuta kufanya hivyo. Hii ni mara ya kwanza rekodi hii kuwekwa na imekuwa ikikua kwa kipindi kirefu.

http://mowwowmedia.com/privacy-policy

Data zilizowekwa wazi na kampuni ya utafiti wa masuala ya utumiaji mtandao ya StatCounter inaonesha watumiaji wa http://rlpattersonart.com/tag/game-of-thrones/ huduma ya intaneti kupitia simu na tableti ni asilimia 51.2 ya watumiaji wote, huku wanaotumia kompyuta ni asilimia 48.7 tuu.
intaneti kupitia simu na kompyuta

Ukuaji wa utumiaji wa intaneti kwenye simu na tableti dhidi ya kwenye kompyuta

Kiwango hichi cha utumiaji kupitia simu na tableti kinakuzwa sana na watumiaji wa huduma ya intaneti kutoka nchi zinazoendelea ambapo ni wachache sana wanamiliki kompyuta ili wengi wao tayari wanamiliki simu za mkononi. Kwa mfano nchini India tuu asilimia 75 ya watumiaji huduma ya intaneti wanafanya hivyo kupitia simu zao. Ingawa nchi zilizoendelea kama vile Marekani na Uingereza bado utumiaji wa kompyuta pia upo juu tayari data zinaonesha asilimia ya utumiaji huo ukizidi kupungua na huku utumiaji wa intaneti kupitia simu za mkononi ukizidi kukua.

Tayari Google pia walitoa data zilizoonesha kufikia mwezi wa tano mwaka huu tayari watu wengi wamekuwa wakitumia huduma yao ya utafutaji, http://reenajbhambra.com/?tag=makeup-technique Google Search, kupitia simu za mkononi kuliko wanaotumia kompyuta kufanya hivyo.

INAYOHUSIANA  Undani wa toleo jipya la Android 9 Pie

Je wewe ni mtumiaji wa intaneti kwa kutumia njia zipi? A) Simu tuu, au B) Kompyuta na simu?

Kumbuka kusambaza makala na pia kuungana nasi kupitia Facebook, Twitter, Instagram, YouTubeTelegram na Google Plus

Vyanzo: StatCounter

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.