Watumiaji wa App Store Watumia zaidi ya Tsh Trilioni 2 (Bilioni $1.1) Kipindi cha Sikukuu

0
Sambaza

Watumiaji wa simu, saa na tableti za Apple watumia zaidi ya trilioni mbili za Kitanzania (Dola Bilioni 1.1 za Kimarekani) katika huduma za App Store katika kipindi cha sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya.

app store apple

Haya ni mapato yaliyopatikana katika kipindi cha wiki mbili, yaani Disemba 20 hadi Januari tarehe 3.

Kwa ujumla wake mwaka 2015 watumiaji wa bidhaa za Apple walitumia dola bilioni 20 za Marekani (zaidi ya Bilioni 43 za TZ) katika huduma za App Store. Huduma hii ni pamoja na manunuzi ya apps na pia utumiaji wa huduma ya malipo ya huduma ya muda mrefu (subscription) na pia ununuaji wa vitu kwenye magemu na app zinginezo.

SOMA PIA:  AirDrop ni nini? Ifahamu njia ya kutuma mafaili kwa haraka kwa watumiaji wa iOS na MacOS

Apple inachukua asilimia 30% ya mauzo yeyote yanayofanywa katika huduma yake ya App Store huku asilimia 70 ikienda kwa watengenezaji Apps

Kuna zaidi ya Apps milioni 1.5 katika soko la apps la App Store

Apple wanajivunia sana kiwango cha ubora wa apps zilizopo katika soko lake la apps na inaonekana wanafanya juhudi zaidi kuhakikisha soko hilo linakuwa kwenye karibia kila aina ya kifaa wanachokuja nacho. Hivi karibuni walikuwa na saa janja ya mkononi ya Apple Watch na sasa tayari apps spesheli za saa hizo zinapatikana katika soko hilo.

SOMA PIA:  Apple yapunguza bei ya betri ya simu zake

Pia hivi karibuni tayari wameanzisha juhudi za kuingiza soko la apps kwenye bidhaa yao kwa ajili ya TV – Apple TV.

Kwa nchini Marekani tuu Apple inadai imesaidia kusababisha ajira zisizo za moja kwa moja za takribani milioni 1.9, hizi zikihusisha watu na makampuni mbalimbali yanayotengeneza na kuuza apps zake katika soko la App Store.

Je ushawahi kulipia app yeyote kwenye simu au tableti yako? Tuambie maoni yako juu ya biashara ya apps za simu.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Leave A Reply

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com