Kama ulituma Tweet yako kwa mara ya kwanza na ukaona haikupata muamko mkubwa au watu wengi hawajaiona basi usiwe na shaka tena
Maboresho yaliyofanywa na kampuni ya Twitter ni kwamba unaweza uka ‘Retweet’ kile ambacho ulikiandika kwa mara ya kwanza
Kuna watumiaji wengine wanaweza wakawa huwa wanapitia vitu mbalimbali ambavyo waliwahi kuvi post katika mtandao huo. Vingine vinakuwaga ni vizuri sana na vingine ni vya kuvunja mbavu, vyote hivi vinaweza vikamshawishi au vikamfanya mtu atamani kuvituma tena kwa mara ya pili.
Now you can easily Retweet or Quote Tweet yourself with just a few taps. Pick an old favorite and give it a try! 🔄 https://t.co/bUj4ezQNOJ
— Twitter (@Twitter) June 14, 2016
Licha ya kutuma tena kwa mara ya pili basi mtu anaweza aka ‘Retweet’ tuu. Twitter waliweka jambo hili wazi jumanne.
Sawa wengine wanaweza wakasema kuwa sio mabadiliko makubwa sana ila kwa mtumiaji mzuri wa Twitter nna uhakika kuwa atakuwa anafurahia sana kipengele hiki
Zamani kile kialama ambacho watu walikuwa wanakitumia kwa kubonyeza ili kuweza ku ‘Retweet’ mtu alichotuma ilikuwa inaonekana kwa watu wale walioku ‘follow’ tuu (Ukifungua tweet yako ilikua huioni ile alama).
Kwa sasa kile kialama unaweza ukakiona hata ukiwa unaangalia Tweet zako za nyuma na hapo ndipo unapoweza kuamua ku ‘Retweet’ ili follower wako waone tena au hata na wale ambao hawakuona waone