Wezi wazima safari ya bajaji inayotumia Nishati ya Jua Ufaransa

0
Sambaza

Safari ya miezi saba ya bajaji inayotumia umeme wa Jua (solar), ambayo ilikuwa inatoka India kwenda hadi Uingereza, imesitishwa kwa muda baada ya wezi kuiba hati ya kusafiria ya dereva wa bajaji hiyo karibu na mji wa Paris.

Mhandisi Naveen Rabelli aliibiwa pasipoti na pochi yake eneo la Sarcelles, alipokuwa ameenda haja. Kwa sasa anasubiri kupata pasipoti mpya ndipo aweze kuvuka English Channel na kuhitimishia safari yake katika Kasri la Buckingham.

Bajaj yenyr kutumia umeme wa jua 'ilitakaswa' kabla yake kuanza safari India

Bajaj yenye kutumia umeme wa jua ‘ilitakaswa’  🙂 kabla ya kuanza safari India

bajaj-umeme-jua

Nia yake kuu ni kujaribu kuwahamaisha watu kutumia nishati mbadala. Safari hiyo imeshachukua miezi saba sasa kutoka nchini India, na maandalizi yake yalichukua miaka minne.

Huwa analala kwenye bajaji hiyo anapokosa mtu wa kumpa malazi. Amefanikiwa kuweka pesa nyingi kwa njia hii. Amepitia Iran, Uturuki, Ugiriki, Bulgaria, Serbia, Austria, Ujerumani na Uswizi.

Bajaj ina kitanda na jiko la sola.

Bajaj ina kitanda na jiko la sola.

Mhandisi huyo alinunua bajaji hiyo $1,500 (£1,120)|Tsh 3,300,000 na akatumia $11,500|Tsh 25,300,000 kuifanyia ukarabati. Kwa sasa, bajaji yake inaweza kufikia kasi ya juu ya 60Km/h (37 mph) na hutumia umeme unaotengenezwa na nishati ya jua.

SOMA PIA:  Tetesi: Kijue chanzo cha kuzuiwa kwa baadhi ya vifaa vya elektroniki katika baadhi ya ndege.

Mhandisi muundaji wa bajaj ni  mkazi wa India lakini ni raia wa Australia na amekuwa akifanyia kazi kampuni ya kuunda magari ya kutumia umeme nchini India.

Vyanzo: BBC, mitandao mbalimbali

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com