Baada ya kipindi kama cha mwezi mmoja WahatsApp ilitangaza kuja na mpango wa kufungua akaunti za kibiashara kwa watumiaji wake sasa tayari wamefungua akaunti hiyo itakayojulikana kama WhatsApp Business.
Kwa ujio wa WhatsApp Business kutasaidia sana wafanyabiashara au kampuni kutenganisha mazungumzo binafsi na yanayohusu biashara na tayari WhatsApp Business tayari inapatikana Play Store kwa watumiaji wa toleo la Beta na ipo katika kipindi cha majaribio ili kupokea maoni ya watumiaji na kurekebisha penye mapungufu.
Uzuri wa WhatsApp Businees unaweza kupanga muda wa kupokea sms kitu ambacho kitapunguza kero kwa kuingia meseji hata usiku wa manane kama ilivyo kwa WhatsApp ya kawaida.
Pia kutakuwa na mipangilio mbalimbali kulingana na biashara yako. Aidha utakuwa unaona idadi ya meseji ulizotumiwa na zile ulizotuma ili kuona muitiko wa wateja wako kwa biashara yako na kufanya tathmini.
Unaweza kuweka picha yako au logo ya kampuni yako ili iwe rahisi kutambulika na wateja wako au wale unaoshirikiana nao katika mambo ya biashara. Inawezesha kuweka mpangilio wa maelezo ya kampuni/biashara yako kama tovuti, anwani/barua pepe na hata kuweka ujumbe maalumu utakaokuwa unajibu wateja wako bila ya wewe kuwepo hewani.