WhatsApp: Desemba 31 2017 ndio mwisho kwa simu janja hizi kufanya kazi! - TeknoKona Teknolojia Tanzania

WhatsApp: Desemba 31 2017 ndio mwisho kwa simu janja hizi kufanya kazi!

0
Sambaza

WhatsApp itaacha kufanya kazi kwa mamilioni ya watumiaji wa simu  janja kadhaa mwishoni mwa mwaka huu kampuni hiyo imethibitisha.

Simu ambazo zitakumbwa na anguko hilo ni zile za mfumo endeshi wa BlackBerry OS, BlackBerry 10, Windows Phone 8.0 na chini ya hapo. Muda wa mwisho uliotolewa awali ulikuwa ni Juni 30 2017 lakini mmiliki wa Facebook ambaye pia ni mmiliki wa whatsApp alisogeza mbele mpaka Desemba 31, 2017.

Desemba 31 2017 ndio siku ya mwisho kwa baadhi ya simu janja kupata huduma ya WhatsApp.

Wakati huohuo simu za Android za toleo 2.3.7 na chini ya hapo zitaacha kupata masahihisho ya WhatsApp mpaka mwaka Februari 1 2020. Aidha simu ya Nokia S40 nayo imesogezwa mpaka Desemba 31, 2018.

INAYOHUSIANA  Pokea na jibu ujumbe mfupi wa maneno kupitia kompyuta

kwa mujibu wa taarifa kutoka WhatsApp wakati wowote kuanzia sasa WhatsApp itaacha kufanya kazi katika simu zilizotajwa.

Orodha kamili ya simu janja zitakazokosa WhatsApp.

buy fluoxetine online >Nokia Symbian S60 mwisho kuanzia juni 30, 2017,
get link >BlackBerry OS na BlackBerry 10 mwisho Desemba 31, 2017,
click >Windows Phone 8.0 na chini ya hapo mwisho Desemba 31, 2017,
>Nokia S40 mwisho Desemba 31, 2018,
>Android Version 2.3.7 na chini ya hapo Mwisho Februari 1, 2018.

WhatsApp imekuwa ikitegemewa na watu wengi kuwasiliana na kupata habari mbalimbali kwa watumiaji wa simu janja. Fanya maaamuzi sahihi sasa.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.