Leo, WhatsApp imetangaza kupitia Twitter kwamba programu yao maarufu ya WhatsApp inatumika kuhudumia ujumbe bilioni 10 kila siku. Kwa undani zaidi kuna takribani ujumbe takribani bilioni 4 zinazoingia na zinazotoka bilioni 6.
WhatsApp Messenger ni programu ambayo inaruhusu kubadilishana ujumbe bila ya kutumia mfumo wa SMS. WhatsApp Messenger inapatikana kwa iPhone, Blackberry, Android, simu za Windows na Nokia na ndiyo, wale wote wanaweza za ujumbe kila mmoja! Kwa sababu WhatsApp inatumia mtandao (intaneti), hakuna gharama kwa ujumbe nje ya gharama za kawaida za intaneti na kama umejiunga na vifurushi vya huduma ya intaneti basi hutakatwa malipo yeyote ya ziada.
Juu ya huduma ya ujumbe mfupi huu, watumiaji wa WhatsApp wanaweza kuunda makundi, kutumiana kila mmoja picha, video na ujumbe wa sauti bila kikomo.
Kwa kushusha (download) tembea www.whatsapp.com au angalia kwenye soko la App la aina ya simu unayotumia!
No Comment! Be the first one.