#AddMe - Link za SnapChat na Telegram Marufuku ndani ya Instagram

Baada ya WhatsApp, Instagram pia Yazuia link za Telegram na Snapchat katika App yao

0
Sambaza

Je unatumia Snapchat au Telegram na unataka kuweka link ya kuwapeleka watu kwenye akaunti yako hiyo kupitia huduma ya WhatsApp au Instagram? Haiwezekani tena.

http://wmswirt.com/wp-json/oembed/1.0/embed?url=http://wmswirt.com/project/sinclair/ Kama adui ananenepa kupitia kula kwako utafanyaje? Mpige marufuku? Inaonekana ndio uamuzi uliochukuliwa na Instagram na WhatsApp dhidi ya link za Telegram

http://trailsandtris.com/tag/brands/ telegram

http://solunayoga.com/classes.html Katika hatua inayoonekana ni kuzuia ukuaji wa huduma shindani huduma ya WhatsApp na sasa Instagram pia ambazo zote zipo chini ya kampuni ya Facebook zimezuia watu kurusha au kuweka link za huduma shindani za SnapChat na Telegram.

Kivipi?

Kwenye WhatsApp ingawa unaweza kuweka link mbalimbali na link hizo zikaweza kubonyezeka ila ukiweka na kutuma kwa mtu ujumbe wenye link inayompeleka mtu kwenye huduma ya Telegram link hiyo haitapokelewa kama link. Inapoteza uwezo wa kuwa link na hivyo kuwa kama ujumbe tuu.

Kutoonekana kwa links za Telegram katika WhatsApp

Kutoonekana kwa links za Telegram katika WhatsApp

Kwa sasa ni watumiaji wa WhatsApp toleo la Android tuu ndio haiwezekani kutuma links za Telegram, inaonekana ni jambo gumu bado kulizuia katika iOS kwa simu za iPhone. Ila watumiaji wa WhatsApp wa Android ni asilimia 80 ya watumiaji wote.

Telegram wakilalamika na kuonesha ukiritimba wa Facebook

Kwenye Instagram watu wengi wamekuwa wakiweka link zao hasa za huduma kama vile Snapchat au Telegram…huku wakiwaambia marafiki wawa-follow/Add kwenye huduma hizo pia. Kuanzia sasa ukiandika link kama ni za Snapchat au Telegram zitakataliwa.

Kutokubaliwa kwa links za telegram katika Instagram wakati za mitandao mingine kama vile Twitter n.k zikikubaliwa

Kutokubaliwa kwa links za telegram katika Instagram wakati za mitandao mingine kama vile Twitter n.k zikikubaliwa

Je ni hofu dhidi ya ushindani?

Kwa kiasi kikubwa wengi wameona suala hilo ni kupunguza kasi ya ukuaji wa Snapchat na Telegram…..hasa hasa ikiwa inaonekana dhahiri huduma hizo zinakua zaidi kupitia watu kuambiana kwa kutumia huduma za WhatsApp na Instagram.

Huduma ya kuchati ya Telegram imezidi kukua na sasa imefikisha wastani wa zaidi ya takribani watumiaji milioni 100 kila mwezi na ikiwa na sifa/uwezo kemukemu zikilinganishwa na zile zinaopatikana katika WhatsApp – Soma makala yetu Je ni App gani ni Zaidi kati ya WhatsApp na Telegram ktk kuchati 

Kwa kiasi kikubwa haileti maana kuona ni huduma hizo tuu ndio zimezuiliwa, huku huduma nyingine zenye mabavu ya kulipizia zikiachiwa – kama vile YouTube, Twitter, LinkedIn n.k. Yote ni mitandao ya kijamii, ila inaonekana hiyo haijaathirika zaidi kwa kuwa haishindani moja kwa moja na huduma za WhatsApp na Instagram.

INAYOHUSIANA  WhatsApp kupambana na taarifa za uongo

Je ni uamuzi ulio sahihi?

Ingawa uamuzi huu unaonekana ni wa kujilinda zaidi kwa WhatsApp na Instagram inaonekana muda si mrefu unaweza ukaingiza kampuni ya Facebook (wamiliki wa WhatsApp na Instagram) matatani. Sheria dhidi ya uhuru katika ushindani katika bara la Ulaya na ata Marekani ni kali sana na inaonekana muda si mrefu kesi dhidi ya WhatsApp na Instagram zinaweza funguliwa.  Watumiaji mbalimbali wa Instagram wameshaanza kuponda uamuzi huo.

Soma Pia – Fahamu nani zaidi kati ya app za WhatsApp na Telegram 

Je wewe ni mtumiaji wa huduma za SnapChat au Telegram na umekuwa ukitangaza akaunti yako kupitia WhatsApp au Instagram? Una maoni gani juu ya uamuzi huu wa WhatsApp na Instagram?

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.