WhatsApp Katika Mchakato Wa Kuongeza Vipengele 2 Vikubwa!

0
Sambaza

Hivi karibuni WhatsApp kwa ajili ya watumiaji wa iOs ilipata maboresho makubwa ambayo mwanzoni hayakuwepo.

Maboresho hayo ni ikiwemo na uwezo wa App hiyo kuweza kuzituma meseji kwa kuziweka kwenye foleni hata kama ukiwa huna intaneti kwa muda huo. Kuweza kuongeza ujazo kwa urahisi kwa kurahisisha kufuta kwa aina za meseji haraka zaidi

Lingine kubwa ni kwamba WhatsApp inawezesha watumiaji wa iOs kuwezo kutumia pich au video nyingi zaidi kwa mkupuo, tofauti na mara ya kwanza ambapo mtu alikuwa anaweza kutuma picha kumi tuu kwa mkupuo. Kwa sasa unaweza kutuma hadi picha 30 kwa mkupuo.

Vipengele Vipya Vinavyosubiriwa Kwa Hamu

SOMA PIA:  Zlatan Ibrahimovic azindua game yake mpya ya Zlatan Legends

Kama kawaida ya App mbalimbali huwa kwanza yanajaribu matoleo yake mapya katika App hizo hizo ila kwa mfumo wa Beta (mfumo wa majaribio). WhatsApp ya mfumo huo tayari inajaribu vipengele viwili ambavyo ni Edit (Hariri) na Recall (jikumbushe)

Jinsi Vipengele Vinavyofanya Kazi
• Edit

Kama mara ya kwanza tulivyoandika kuhusiana na kipegele cha Edit hapa. Kipengele hiki kazi yake kubwa itakuwa ni kuweza kuhariri ujumbe ambao tayari umeshatumwa. Yaani kama ulishatuma ujumbe huo unaweza ukauvuta na kuubadilisha au kuuboresha. Kitu kimoja ambacho kinahitajika ila kuliwezesha jambo hili ni kwamba inabidi ujumbe huo uwe bado haujasomwa na mtu anaetumiwa. Kama akiusoma tuu zoezi litashindikana.

Kipengele Cha Edit

Kipengele hiki kitapokelewa kwa mikono miwili na watumiaji ambao mara kwa mara huo wanatuma ujumbe alaf u baadae wanajilaumu na kutamani kuwa wangeweza kuwa na uwezo wa kubadilisha ujumbe huo
• Recall/Revoke 

Kipengele hiki kitaifanya meseji ambayo imetumwa lakini haijasomwa ikurudie wewe ulieituma. Yaani kule inajifuta inakuwa kama hukutuma mara ya kwanza.

SOMA PIA:  Uber Sasa Inaruhusu Kuomba Usafiri Kwa Ajili Ya Mtu Mwingine!

Kipengele hichi ni cha muhimu hebu fikiri kwa mfano umetoka kupiga moja moto na moja baridi na zikapanda kichwani ukachukua simu yako na kumuandikia meseji nzito bosi wako. Asubuhi ikafika na pombe zikawa zimeshaanza kutoka kichwani kama bado bosi wako hakufungua meseji yako basi una uwezo wa kuivuta kwako na bosi hataiona tena.

kipengele Cha Recall/Revoke

Vipengele hivi vyote viwili kwa sasa vinapatikana katika toleo la WhatsApp la Beta kwa watumiaji wengine haina budi kusubiri mpaka pale WhatsApp hii itakapoweza kupatikana kwa kila mtu.

SOMA PIA:  Mauzo ya iPhone 8 na iPhone 8 Plus yadorora

Haifahamiki dhahiri juu ya siku ambayo WhatsApp wataachia vipengele hivi kwa kila mtu lakini ni kwamba taarifa zilizopo ni hivi karibuni siku yeyote kuanzia sasa.

Ningependa kusikia kutoka kwako niandikie hapo chini sehemu ya comment je hili umelipokeaje?

Kumbuka kusambaza makala na pia kuungana nasi kupitia Facebook, Twitter, Instagram, YouTubeTelegram na Google Plus

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa Teknokona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com