WhatsApp kuacha ku-support OS za Nokia na Blackberry.

0
Sambaza

WhatsApp Imesema kwamba itasitisha uungaji mkono kwa baadhi ya OS ambazo haizumiki tena ama ambazo zinatumiwa na watumiaji wachache zaidi, OS kama Blackberry 10, Nokia Symbian S60 na Windows Phone 7.1 ni moja ya OS ambazo zitasitishiwa uungaji mkono.

Pia Whatsapp  itasitisha uungaji mkono kwa matoleo ya awali kabisa ya OS ya Android 2.1 na 2.2.

Wakati WhatsApp inaanza mwaka 2009 simu janja hazikuwa zimeshika kasi kama ilivyo sasa, kwa wakati ule simu zilizokuwa maarufu zaidi na ambazo zilikuwa zinapatikana kwa wingi zaidi ni zile za Nokia na Blackberry. Leo miaka 6 baadaye asilimia 99.5 ya simu zinazotengenezwa zinatumia OS za Android ama iOS ama Windows, hii ni wazi kwamba zama zimebadilika na mabadiliko hayakwepeki.

SOMA PIA:  Sasa unaweza kuagiza chakula Facebook.

OS za Nokia na Blackberry

Hii inamaana gani kwa wanaotumia simu zenye OS hii?!

WhatsApp kusitisha uungaji mkono kwa OS hii inamaanisha kwamba matoleo ambayo yanafuata ya app ya WhatsApp hayaweza kutumiwa kwa kutumia vifaa hivi ama hata yakiweza kutumika basi hayatakuwa na uwezo kamilifu katika vifaa vyenye hizi OS.

Je kwa watumiaji wa WhatsApp ambao wanatumia vifaa vyenye OS hizi wafanye nini?

Kusitishwa ungaji mkono wa watengenezaji wa app haina maana kwamba matoleo ya zamani ya app hiyo hayataweza kufanya kazi katika vifaa, hii inamana kwamba wamiliki wa vifaa ambayvo vina OS tajwa wanachotakiwa ni kuendelea kutumia matoleo ya WhatsApp ya zamani na kuto shiriki katika ku-update WhatsApp kwa maana matoleo yanayofuata baada ya January 2017 maana matoleo haya yanaweza shindwa kufanya kazi katika simu yako ama yakafanya kazi ila kwa kusumbua.

SOMA PIA:  YouTube GO - App ya YouTube isiyokula data sana

WhatsApp wanasema wanafanya hivyo ili waweze kuiboresha app yao na vifaa ambavyo vinaendeshwa na hizo OS tajwa havitaweza kuyapokea mabadiliko hayo kwa kuwa zimepitwa na wakati.

Inategemewa kwamba kunatoleo jipya la WhatsApp linakuja baadaye mwaka huu ambalo pamoja na mambo mengine litaboresha hasa mambo ya kiusalama ya app hiyo, utakumbuka kwamba usalama ni agenda namba moja kwa mitandao mingi ikiwamo na mtandao huu ambao hivi karibuni ulifikisha watumiaji bilioni moja.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com