WhatsApp kutotuma data za watumiaji wake kwenda Facebook kwa sasa ni kitu cha uhakika kwa watumiaji wa baadhi ya nchi.
Uwamuzi wa Facebook kununua app hii maarufu mwaka 2014 ulichukuliwa na wengi kuwa lengo kuu ni kwa Facebook kuona jinsi ya kutumia data zinazowahusu mamilioni ya watumiaji.
Na kuna kipindi kulifanyika mabadiliko machache kwenye app hiyo yaliyoonesha mwanzo wa Facebook kutaka kuanza kupata data za watumiaji wa app hiyo – watu wengi walilalamika sana na ndio ikaleta chunguzi nyingi kutoka vyombo vya usalama wa data vya serikali mbalimbali ikiwemo ya Uingereza.
Chombo cha serikali ya Uingereza kinachohusiana na taarifa, ICO – Information Commissioner’s Office, kilifungua uchunguzi kama WhatsApp wanatuma data kuhusu watumiaji wake kwenda tovuti ya Facebook. ICO walidai kufanya hivyo kungekuwa ni uvunjifu wa sheria na mkataba katika ya app ya WhatsApp na mamilioni ya watumiaji wake.
ICO imekuja na matokeo ikisema imejiridhisha kabisa ya kuwa kwa sasa app ya WhatsApp haitumi data za watumiaji wake kwenda kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook.