WhatsApp kwenye iPad ipo mbioni kupatikana

0
Sambaza

Kifaa kama iPad kuwa na WhatsApp kwa miaka mingi sana imeonekana kuwa ni jambo ambalo kama watumiaji wa iPad walisahaulika lakini la hasha! Mambo mazuri yanakuja kwa wenye iPad.

Inaaminika kwa watu ambao wana iPad huwenda nao wakawa na uwezo wa kutumia app hiyo (WhatsApp) yenye watumiaji wengi sana ulimwenguni kote na inayomilikiwa na Facebook.

Habari hizi zinaonekana kuwa ni za uvumi lakini zina ukweli mkubwa ndani yake kwani kwenye toleo la hivi sasa laWhatsApp Desktop 0.2.6968 kuna kipengele kinachoashiria mtu anaweza kuunganisha WhatsApp ya kwenye iPad hadi kwenye kivinjari.

Inawezekana kama ikawa imekosewa kwa kuandikwa Tablet-iOS na sote tunajua kuwa chochote kinachotumia iOS ni iPhone, iPod/iPad.

Wachambuzi mbalimbali wanaamini kuwa WhatsApp wana mpango wa kuleta WhatsApp kwenye iPad na hivyo kukata kiu ya wengi kutokana na kifaa hicho huko nyuma ilikuwa ni ngumu kufikiria kama kulikuwa na mipango yoyote ya kufanya kifaa hicho kiwe na uwezo wa kukubali WhatsApp.

Kwa wiki kadhaa sasa WhatsApp imekuwa ikileta vitu vipya kwenye WhatsApp na kutokea kupendwa vilivyo; kwa uchache tu vitu kama WhatsApp4Business, simu/video kwenye kundi la WhatsApp, Live Location, n.k.

WhatsApp kwenye iPad? 🙄 🙄 Hakika hii ni habari njema na ya kuvutia jambo ambalo linaweza likaongeza kasi ya watu kununua iPad kwa sababu sasa wataweza kutumia programu tumishi maarufu zaidi duniani kuweza kuwasiliana na watu.

Vyanzo: Gadgets 360, WABetaInfo

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
SOMA PIA:  Marekani: Kirusi cha WannaCry kimetoka Korea Kaskazini
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com