Kuna uwezekano wa WhatsApp Na Facebook Kuunganishwa, Nini Nyuma Ya Pazia?

0
Sambaza

Kipindi ambacho Facebook ilinunua WhatsApp mwaka 2014 kwa dola za kimarekani bilioni 19, watu wengi na wadau wa teknolojia walikuwa na swali moja la kujiuliza nalo ni Kwa nini Facebook wamenenua mtandao huo?

Hakukuwa na sababu ya Facebook na WhatsApp kumilikiwa na mtu mmoja na kuwa chini ya kampuni ya Facebook. Lakini hata hivyo kulikuwa na baadhi ya maeneo yanayoonyesha kuwa hizi mbili kidogo zinaendana.

Kwa taratibu Facebook inaonyesha kuwa inashughulika katika kuziweka Facebook na WhatsApp karibu

Chati ikionyesha Ukuaji Wa Watumizi Wa Mtandao Wa WhatsApp

Chati ikionyesha Ukuaji Wa Watumizi Wa Mtandao Wa WhatsApp

Taarifa iliyovuja ni kwamba katika toleo jipya la WhatsApp kutakuwa na ruhusa ya mawasiliano kati ya mtandao wa Whatsapp na mtandao wa Facebook . Wataalamu  walipokuwa wakicheza na teknolojia ya kuroot simu katika Android waligundua kuwa toleo la whatsApp lile la 2.12.413 lilionyesha kuwa kuna chaguo la kuunganisha WhatsApp na Facebook kwa lengo la ‘kukuza uzoefu wa kutumia Facebook’

Toleo hilo likionesha uwezo wa kuunganisha akaunti ya WhatsApp na Facebook

Toleo hilo likionesha uwezo wa kuunganisha akaunti ya WhatsApp na Facebook

Licha ya kuwa matumizi kamili ya maunganisho haya bado hajajulikana kwa uhakika. Inaweza ikawa kwamba whatsapp inawaruhusu watumiaji wake kuweza kupost vitu Facebook wakiwa katika WhatsApp. Au pengine matumizi sahihi ya muunganiko huu yatajulikana pale muungano huu utakapoanza kufanya kazi.

SOMA PIA:  Watu wawili tu ndio hutaweza kuwa'bloku' facebook!

Lakini pia kitu kimoja ambacho ni cha uhakika ni kwamba kwa kipindi kijacho mtumiaji wa WhatsApp atakuwa na uwezo wa kupost katika mtandao wake wa Facebook na WhatsApp akiwa katika moja ya mitandao hiyo.

Mtandao wa WhatsApp ambao ndio mkubwa katika App zile za kutuma na kupokea meseji imeripotiwa kuwa mtandao huo upo katika matayarisho ya kuweza kutumia mtandao huo kupiga simu  za kuonana uso kwa uso kama vile Skype. Lakini pia kumbuka ilipiga chini tozo zake za mwaka (dola 0.99)

SOMA PIA:  Viongozi wa makundi WhatsApp 'kuongezewa nguvu'

Tuambie wewe unahisi nini ambacho unakitarajia kutokea kutokana na muunganiko huu, tuandikie sehemu ya comment hapo chini. Pia usisahau kutembelea mtandao wako pendwa wa teknokona kila siku. Kumbuka TeknoKona Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!

Vyanzo: GSMArena na vyanzo vinginevyo

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa Teknokona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Leave A Reply

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com