Whatsapp yaboreshwa; Sasa unaweza kuchora kitu chochote kwenye picha/video

1
Sambaza

Siku zote katika biashara lazima uwe mjanja ili kuweza kuendelea kuwavutia wateja wako au hata kupata wateja wapya kutokana na ubora wa bidhaa zako; WhatsApp wameliona hilo na wao wameamua kuiboresha app yao.

whatsapp yaboreshwa app

Ulikuwa ukitamani kuona unaweza kuchora kitu chochote kwenye picha/video kabla ya kumtumia mtu/watu au hata kuiweka kama picha ya kuweza watu kukufahamu wewe ‘Display picture’ almaarufu kama dp? Basi sasa unaweza kufanya hivyo kwenye whatsapp.

Kuweza kuchora kitu kwenye picha si jambo geni kwa watumiaji wa Snapchat na kwa hivi kari buni kwenye Instagram na iMessage.

 Jinsi ya kuweza kupata maboresho mapya kwenye Whatsapp

Kwenye app yoyote ile ili kuweza kupata maboresho inapaswa programu tumishi iwe ni ya toleo jipya (latest version). Baada ya hapo utakapojaribu kuchagua au video basi kabla ya kuituma utaweza kuandika (caption)/kuchora kitu chochote katika picha au video hiyo.

SOMA PIA:  CCleaner: Programu muhimu ya kusafisha kompyuta iliyogeuka kuwa kirusi

Unaweza ukabadilisha rangi halisi ya picha na kuwa yenye rangi ya mpauko; kama picha za miaka ya nyumawakati kamera zilikuwa hazijafanya maugeuzi katika uboreshwaji wa picha inayopigwa kwenye kamera yenyewe.

Baadhi ya vitu unavyoweza weka kwenye picha

Maboresho hayo ni mazuri na ni jambo la kuvutia kwani sasa unaweza ukaongezea mvuto wa picha au kuharibu kabisa kutokana na kile ulichokiandika au kukichora kwenda kwa mpokeaji wa picha.

Ni muhimu kutumia maboresho haya kwenye Whatsapp katika namna njema ambayo haitamkwaza mpokeaji/wapokeaji wa picha husika.

Kumbuka kusambaza makala na pia kuungana nasi kupitia Facebook, Twitter, Instagram, YouTube, Telegram na Google Plus

Vyanzo: Telegraph, iNews

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com