WhatsApp Yafikisha Watumiaji Milioni 700 kwa Mwezi!

0
Sambaza

WhatsApp inazidi kukua kwa kasi na Facebook wanaringa kwelikweli kwani wanajitahidi kuwaonesha wawekazaji ya kwamba uamuzi wa kununua kampuni hiyo ya WhatsApp ulikuwa muhimu na wenye faida.

Katika kuonesha hili Facebook wamekuwa na utamaduni wa kuonesha data mbalimbali zikionesha ukuaji wa mtandao huo na mwezi huu wameonesha data zao za ukuaji.

is viagra safe long term whatsapp_tanzaniaData hizo zinaonesha watumiaji wa WhatsApp kwa mwezi umepanda kutoka wastani wa takribani watumiaji milioni 600 hadi kwenda watumiaji milioni 700 kwa sasa.

SOMA PIA:  Sasa unaweza kuagiza chakula Facebook.

Hii inaonesha ukuaji wa takribani watumiaji milioni 200 tokea Facebook waliponunua kampuni hii.

Kwa sasa kuna wastani wa meseji bilioni 30 zinatumwa kila siku kutumia WhatsApp.

Ukuaji wake katika wastani wa watumiaji wa huduma kwa mwenzi umeifanya WhatsApp kuwa kileleni kuzidi huduma zingine za kijamii kama vile Twitter (Watumiaji milioni 284 kwa mwezi) na Instagram ikiwa na watumiaji milioni 300 kwa mwezi wa Disemba 2014. Kwa sasa WhatsApp imepitwa na Facebook, kampuni mama, ikiwa na wastani wa watumiaji bilioni 1.3 kila mwezi.

SOMA PIA:  Apps mbalimbali katika simu moja kwa akaunti mbilimbili

Fahamu mambo na ujanja mbalimbali katika kutumia WhatsApp -> HAPA!

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Leave A Reply

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com