Whatsapp Yapata Muonekano Mpya wa ‘Material Design’

0
Sambaza

WhatsApp, huduma maarufu ya ujumbe-pupa imepata maboresho yaliyokuwa yakisubiriwa na wengi –  muonekano mpya wa ‘Material Design’ kwenye Android. Material Design ni muongozo mpya wa muonekano wa Android na programu zake kwa mujibu wa Android, toleo la 5.0.

Muongozo huo unaleta mbadiliko ya kimuonekano kama kupanga vitu ki-gridi zaidi, kuongeza manjonjo wakati wa kufungua/ kufunga app na ‘effect’ za rangi na vivuli kwenye muonekano wa app.

Mabadiliko haya yameibadilisha sana WhatsApp kama tulivyoizoea na unaweza kujionea mwenyewe kwa mifano hii chache ya picha:

wpid-2015-04-14-23.11.30.png.png

Skrini ya mwanzo ukifungua WhatsApp

wpid-screenshot_2015-04-14-22-56-53.png

Skrini ya kuandika ujumbe

wpid-2015-04-14-22.59.01.png.png

Taarifa za unayemuadikia ujumbe zinaonekana kama hivi.

Na ukitaka kuongeza picha, video au namba kwenye ujumbe..

Na ukitaka kuongeza picha, video au namba kwenye ujumbe..

Toleo hili jipya la WhatsApp linategemewa kumfika kila mtu anayeitumia kwenye simu za Androidi kupitia Google Playstore ndani ya siku chache zijazo lakini kama unataka kuipata sasa hivi, ingia moja kwa moja kwenye kurasa yao->> hii hapa, ishushe na kupakia kwenye simi yako ya Android.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
SOMA PIA:  Namna ya kuwa WhatsApp Tester (Tumia toleo la beta) #Maujanja
Share.

About Author

Ninafuatilia teknolojia kila siku na ninapenda kutoa ujuzi wangu kuhusu teknolojia. Karibu tuzungumze kuhusu teknolojia hapa teknokona!

Leave A Reply

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com