Wiki ya Ubunifu chini ya Shirika la HDIF Yaanza Rasmi! #InnovationTZ

1
Sambaza

Wiki ya ubunifu (Innovation) chini ya ufadhili wa shirika la HDIF (HUMAN DEVELOPMENT INNOVATION FUND) imeanza rasmi jijini Dar es Salaam.

Itahusisha shughuli mbalimbali hii ikiwa ni pamoja na utambulishwaji wa miradi iliyojishindia ufadhili kutoka shirika hilo lisilo la kiserikali.

HDIF Innovation Week Dar es Salaam

Katika wiki hii kutakuwa na shughuli mbalimbali zinazohusisha wiki waliyoipa jina la Innovation Week, yaani wiki ya Ubunifu. Moja ya shughuli kuu itakuwa ni pamoja na utambulisho wa miradi 14 mipya inayonufaika na uwezeshwaji kutoka mfuko wa uwezeshaji wa HDIF.

SOMA PIA:  Roketi ya Space X yatumika kwa zaidi ya safari moja! #Anga

Kuna shughuli zilizowahi kwa wote na kama ungependa kuhudhuria unaweza angalia ratiba kupitia hapa – Ratiba HDIF Innovation Week.

Je ni aina gani ya miradi inapata msaada?

Ili kunufaika na fedha hizi za msaada, taasisi sharti ionyeshe ubunifu, mradi uwe na mchango kwa maendeleo, mradi uwe na mwelekeo unaoeleweka, na uwezo wa taasisi husika kuufanikisha mradi wenyewe.

“Tangu mfuko wa HDIF uanzishwe mwezi wa tisa 2O13, Tanzania imepaa kwenye orodha ya nchi za teknolojia kutoka 123 duniani hadi 117 kati ya 142 zilizotafitiwa. Ubunifu unahitaji tuwe kijiji ili ufanikiwe,”

Lengo la Wiki ya Ubunifu (Innovation Week)

Naibu Kiongozi wa Shirika la HDIF Bwana Joseph Marinakiza anasema inalenga kuwaleta pamoja wale wote wenye miradi na wale ambao wanaweza kuwawezesha. Na ni kupitia wiki hii mambo kama vile mafanikio na changamoto mbalimbali katika eneo la ubunifu huzungumzwa.

SOMA PIA:  Miundombinu ya TEHAMA na intaneti nchini Tanzania #Uchambuzi #Ripoti

Taasisi zingine zinazohusika na Wiki ya Ubunifu ni Kinu Innovation Hub, Deloitte, Ubalozi wa Finland, Buni Innovation Hub, Tanzania Renewable Energy Incubator, na Ifakara Health Institute.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com