WileyFox: Kampuni ya simu inayotaka kunufaika na uamuzi wa Uingereza kutoka EU

0
Sambaza

WileyFox ni kampuni mpya inayojishughulisha na utengenezaji na uuzaji wa simu janja nchini Uingereza.

Mwaka jana kampuni ijulikanayo kama WileyFox ilizindua simu janja zinazotengenenezwa na kampuni hiyo. Kampuni hiyo ni mpya yenye makao makuu yake nchini Uingereza. Uingereza sio maarufu kwa utengenezaji wa simu janja lakini WileyFox wameonekana kutaka kufanya wajulikane ndani na nje ya Uingereza kwa utengenezaji wa simu janja.

Simu janja zinazotengenezwa na WileyFox

Simu janja zinazotengenezwa na WileyFox

Mwaka jana kampuni hiyo ilizindua matoleo mawili ya simu janja: WileyFox Swift na WileyFox Storm kati ya mwezi Septemba na Oktoba mwaka jana.

WileyFox Swift ina kamera yenye 13 megapixels, 5 megapixels kwa kamera ya mbele na pia inatumia simcard mbili, betri yake inaweza kutoka, ina sehemu ya kuweka SD card. Inauzwa £129 (Takribani Tsh 370,000/=).

WileyFox Swift

WileyFox Swift

Huku WileyFox Storm ikiwa na kamera yenye 20 megapixels, 8 megapixels kwa kamera ya mbele(selfie) na kioo chenye urefu wa inchi 5.5 na inauzwa £199 (Tsh 570,000/=).

Simu janja hizo zinatumia toleo spesheli la programu endeshaji ya Andoid ya familia ya Cyanogen.

WileyFox Storm specifications

WileyFox Storm specifications

Mmiliki wa kampuni hiyo Bw. Nick Muir amesema kuwa kampuni yake haitegemei kupata hasara kutokana na Uingereza kujitoa EU kwani wao tayari wana soko China na kwingineko na bidhaa zao zinaaminika na kupendwa ndani na nje ya Uingereza. Pia wana mpango wa kutanua biashara yao nchini Italia, Ufaransa, Ujerumani na Hispania.

SOMA PIA:  Tetesi: Kijue chanzo cha kuzuiwa kwa baadhi ya vifaa vya elektroniki katika baadhi ya ndege.

Kama makampuni mengine yanayokuwa kwa kasi ya nchini China, kampuni hii inategemea kuuza simu zake kupitia njia ya mtandao tuu. Hii inasaidia kupunguza gharama mbalimbali na hivyo kuhakikisha simu zao zinakuwa za bei nafuu zaidi.

Bw. Nick Muir aliyeacha kazi Motorola baada ya kufanya kazi kwa karibu muongo mmoja na kuanzisha kampuni yake mwenyewe

Bw. Nick Muir aliyeacha kazi Motorola baada ya kufanya kazi kwa karibu muongo mmoja na kuanzisha kampuni yake mwenyewe

Tangu kampuni hiyo ianze kutengeneza simu janja imetengeneza simu janja zaidi ya laki mbili na nusu na kuziuza kupitia Amazon na kampuni hiyo imetoa toleo lake la tatu Juni 28 mwaka jana ambapo simu janja hiyo ina maboresho mengi na inauzwa £200 (Tsh 373,000/=). Wao kama kampuni watatanua wigo wa biashara na kuanza kuuza simu zao Mashariki ya Kati pamoja na Afrika.

SOMA PIA:  Teknolojia ya FaceID kwenye iPhone X 'yamvuruga' John Cena

Je, una la ziada ungependa Teknokona tukufahamishe kuhusiana na simu janja hii kutoka Uingereza? Tuambie katika comment nasi tutashughulikia maoni yako/swali lako.

Chanzo: The Teelgraph, AndroidCentral

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia.

Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com