Kampuni ya simu ya Xiaomi, June 24 imezindua simu yake mpya Redmi 6 pro huko nchini Uchina ikiwa na prosesa ya kisasa na yenye kasi ya Octa-core Snapdragon 625 ikiuzwa kwa bei rahisi zaidi.
Redmi 6 pro inakuja na kioo cha ukubwa wa inchi 5.84 (19:9) chenye mng’ao wa 2280×1080 (FHD) pamoja na ukubwa wa RAM 4GB na uhifadhi wa ndani wenye ukubwa wa 64GB pamoja na kuweza kuweka memori kadi mpaka ukubwa wa 256GB.
Kwa upande wa kamera inakuja na kamera mbili za nyuma moja ikiwa na 12MP na nyingine ikiwa 5MP. Kwa upande wa kamera ya mbele ina 5MP na uwezo wa kuingiza mwanga wa kutosha kwenye lenzi kwa f/2.2.
Redmi itakuwa na inaendeshwa na mfumo wa Android 8.1 uliboreshwa kwa MIUI 9, simu hiyo itakuwa na ukubwa wa betri lenye ujazo wa 4000mAh ambapo inakuhakikishia kutokuwa na matatizo ya kutembea na chaji ya ziada (Power Bank).
Simu hiyo inakuja na rangi Nyeusi, Udhurungi, Bluu, Nyekundu na Dhahabu, itaanzwa kuuzwa karibuni kwa bei zifuatazo:-
3GB RAM/32GB Memori ya ndani: Dola 153 sawa na shilingi 348,075
4GB RAM/32 GB Memori ya ndani: Dola 184 sawa na shilingi 418,600
4GB RAM/64 GB Memori ya ndani: Dola 199 sawa na shilingi 452,725Sifa za Xiaomi Redmi 6 Pro kwa uchache
Kioo
Aina: IPS LCD
Ukubwa: inchi 5.84
Mng’ao: 1080 x 2280 pixels, uwiano wa 19:9Jukwaa
Prosesa: Qualcomm MSM8953 Snapdragon 625
Kasi:Octa-core 2.0 GHz Cortex-A53Uhifadhi
Wa ndani: 32/64 GB
Nje: hadi memori ya ukubwa wa 256GB
RAM: 4GB au 3GBMawasiliano
Teknolojia: 2G, 3G, 4G
Kadi za simu: Laini mbiliKamera
Ya nyuma: 12MP na 5MP
Ya mbele: 5MPBetri
Ukubwa: 4000mAh
Aina: Li-Po