Xiaomi ‘yaikaba koo’ Samsung katika soko la India

0
Sambaza

Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na Counterpoint, simu za Xiaomi zimeongeza sehemu kubwa ya soko lake nchini India katika robo tatu ya mauzo yake katika mwaka huu na kubakisha pengo dogo na simu za Samsung.

Xiaomi zimeuza kwa asilimia 22 ya simu zote zilizouzwa nchini India katika robo tatu ya 2017 ambapo robo tatu ya mwaka uliopita iliuza kwa asilimia sita pekee. Hii inamaanisha mauzo ya simu za Xiaomi yamepanda sana kulinganisha na Samsung ambao wamebaki katika asilimia 23 ya mauzo ya robo tatu kwa mwaka jana na mwaka huu pia.

Takwimu za mauzo ya simu kwa makampuni mbalimbali. Xiami na Samsung kwa pamoja inachangia 45% ya mauzo yote ya simu janja nchni India.

Kupanda kwa mauzo ya Xiaomi kumechagizwa sana kwa ubora wake na bei yake nafuu ambapo kwa soko la India ni muhimu na huzingatiwa sana. Takwimu zinaonesha kwamba Samsung itahitaji mabadiliko fulani ikiwa inataka kubaki juu kwenye soko la India, vinginevyo katika robo ya nne ya mwaka huu Xiaomi inaweza kuongoza mbele ya Samsung.

Xiaomi ni kampuni ya kichina yenye makao yake makuu huko Beijing inatajwa kama kampuni ya tano kwa uzalishaji wa simu duniani. Mbali na kutengeneza simu pia inatengeneza Laptop, vifaa vya elektroni na App mbalimbali.

Majina ya simu za Xiaomi yana familia mbili moja Mi na nyingine Mi note, ambapo simu za karibuni kutoka familia hizo ni Mi Note 3,Mi Note 2, Mi 6, Mi 5c na nyingine nyingi.

Simu janja ya Xiaomi Mi note 3

Kampuni Xiaomi Inc ilianzishwa April mwaka 2010 na simu janja yake ya kwanza ilitolewa mwaka 2011. Mwanzilishi wake anajulikana kama Lei Jun na kwa mujibu wa Forbes ni tajiri namba 23 duniani.

xiaomi

Xiaomi wana bidhaa mbalimbali za kielektroniki, ila kama kampuni bado hawajasambaa sana kwenye soko la Afrika

Simu za Xiaomi kwa soko la Tanzania ni dogo sana kulinganisha na simu zingine kiasi kwa watu wengi ni jina geni. Kwa wauzaji simu ni vyema kuanza kuziuza kwani ni simu imara, bora na bei yake ni nafuu.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
SOMA PIA:  Jicho Letu Katika TECNO Phantom 8 Na Samsung Galaxy Note 8!
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com