Xiaomi yaizidi Samsung katika mauzo ya soko la India

0
Sambaza

Baada ya kuikaba koo kwenye mauzo ya robo tatu ya mwaka 2017, hatimaye simu za Xiaomi zimezidi simu za Samsung katika mauzo ya robo ya nne ya mwaka 2017 kwa soko la India.

Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na kampuni ya Counterpoint inayofanya kazi za utafiti na takwimu imeonesha simu za Xiaomi zimeuzwa zaidi kuliko za Samsung katika robo ya nne ya mwaka 2017.

Ripoti hiyo inaonesha Xiaomi wameuza simu zao kwa asilimia 25 mbele ya Samsung ambao wameuza kwa asilimia 23 katika robo ya nne ya mwaka 2017.

Xiomi na Samdung kwenye mauzo: Xiaomi yaizidi Samsung kimauzo nchini India.

Mauzo ya Xiaomi yamepanda kwa asilimia 3 ambapo Samsung wamebaki katika mauzo yaleyale ya robo ya tatu ya mwaka 2017. Katika robo tatu ya mwaka 2017 Xiaomi waliuza kwa asilimia 22 nyuma ya Samsung waliouza kwa asilimia 23.

Kwa mwaka 2016 katika robo ya nne Xiaomi waliuza asilimia 9 tu ambapo Samsung waliuza kwa asilimia 24. Simu za Xiaomi zimeendelea kupendwa na kununuliwa kwa wingi kutokana na ubora wake na unafuu wa bei yake.

xiaomi

Bidhaa mbalimbali za Xiaomi.

Xiaomi kuongoza kwenye soko la India kuna maana kubwa sana kwa ustawi wa simu zake kwani India ni soko la pili kwa ukubwa badala ya lile la Uchina. Je, wewe unatumia simu/bidhaa nyingine za Xiaomi?

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
SOMA PIA:  Toleo La ''Nokia 6'' Lauzika Ndani Ya Dakika Moja!
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com