Yahoo: Taarifa za akaunti bilioni 1 zadukuliwa

0
Sambaza

Kwa Yahoo inaonekana majanga ya kudukuliwa taarifa za watumiaji wake hayaishi. Mwezi Septemba tuu kulikuwa na taarifa za udukuzi wa mamilioni ya akaunti na sasa watoa taarifa inayoonesha wamedukuliwa tena na taarifa za akaunti bilioni 1 zadukuliwa.

akaunti bilioni 1 za Yahoo zadukuliwa

see Je akaunti yako ipo salama?

is it illegal to buy propecia online Mwezi Septemba taarifa iliyotolewa ilionesha takribani taarifa za watumiaji milioni 500 wa Yahoo zilidukuliwa ndani ya mwaka 2014. Jumatano hii Yahoo wamekuja tena na kusema kuna udukuzi mwingine uliofanyika mwezi wa nane mwaka 2013 na ulihusisha udukuzi wa taarifa bilioni 1 za watumiaji wa mtandao huo maarufu.

Yahoo inashauri watumiaji wake wote ambao hawajafanya mabadiliko ya nywila zao (password) kufanya hivyo mara moja.

INAYOHUSIANA  Marufuku ya matumizi ya mitandao ya kijamii

TeknoKona inakushauri vipi?

Tunakushauri ubadilishe pia password za kwenye akaunti zako nyingine zozote ambazo zinafanana na ile unayoitumia kwenye huduma za Yahoo.

Je unafahamu jinsi ya kutengeneza nywila iliyo salama zaidi? Soma makala yetu hapa – Jinsi Ya Kutengeneza Neno Siri (Password) Imara!

 

Ni muhimu sana kuhakikisha unabadilisha mara kwa mara nywila (password) unazotumia mtandaoni.

Kumbuka kusambaza makala na pia kuungana nasi kupitia Facebook, Twitter, Instagram, YouTubeTelegram na Google Plus

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.