Mambo Makubwa Yaliyotangazwa Katika Tukio La Uzinduzi Wa iPhone 7!

Mambo Makubwa Yaliyotangazwa Katika Tukio La Uzinduzi Wa iPhone 7!

2
Sambaza

Kama kwa namna moja ua nyingne hukuweza kupata muda wa kutosha katika kupata taarifa za hapa na pale kuhusiana na tukio zima la uzinduzi wa iPhone 7 usijali kabisa.

TeknoKona kama kawaida yake tunakuchambulia yale ambayo yana umuhimu sana na yalitajwa katika tukio zima la Apple la uzinduzi wake wa iPhone 7.

http://dazzlingdwelling.com/2015/08/10/pressure-wash-your-home/ Sifa Za iPhone 7

http://kodakey.com/surviving-motorcycle-accident/ NETWORK – GSM/ CDMA/ HSPA/ EVDO/ LTE

http://maxwell3d.net/media_category/tata-water-tanker/ LAINI – Simu Inatumia ile laini ndogo kabisa maarufu kama ‘Nano Sim Card’

KIOO – Kina ubora wa LED ambacho ukubwa wake ni 750 x 1334 pixels. Kingine ni kwamba kioo hichi kina uwezo wa ‘3D Touch’

OS – iOS 10

CPU – Quad Core

MEMORY  –  Memori yake ya ndani inayokuja nayo ni GB 32/128/256 na Ram ya GB 2

KAMERA – Kamera yake ya mbele ni MP 7 wakati ya mbele ni MP 12

BETRI – Inakaa mpaka masaa 14 (ukiwa unaongea huku iko katika 3G). Inakaa Mpaka masaa 40 ukiwa unacheza muziki tuu

 Sifa Za iPhone 7 Plus

Sifa zake ni kama za iPhone 7 tuu lakini hivi vifuatavyo ndio vimebadilika

KIOO – Kina ubora wa LED ambacho ukubwa wake ni 1080 x 1920 pixels. Kingine ni kwamba kioo hichi kina uwezo wa ‘3D Touch’

RAM –  Uwezo wa RAM GB 3

BETRI – Inakaa mpaka masaa 384 (ikiwa katika 3G), Mpaka Masaa 21 (ukiwa unaongea nayo na ikiwa katika 3G), Mpaka Masaa 64 ukiwa unacheza muziki tuu

INAYOHUSIANA  iPhone X yadumu kwa wiki mbili chini ya mto

 

Kubwa ambalo nadhani karibia kila mtu atakuwa analifahamu ni kwamba simu hizo zinakuja bila ya kuwa na tundu la kuingiza spika za masikio (Earphone/Headphone) – Soma Zaidi hapa.

Spika Mpya Za Masikioni Zinazokuja Na Simu Za Matoleo Ya iPhone 7

Lakini hilo sio jambo pekee tuu ambalo lilikuwa la aina yake mengine ni kama vile :-

1. Jinsi Ya Kuunganisha Spika Za Masikio (Earphone/Headphone)

iPhone 7

Kebo Spesheli Ya Kuunganisha Spika Za Masikioni Katika Simu Ya iPhone

Kama inavyojulikana ni kwamba kampuni limeamua kuondoa tundu la spika za masikio katika simu hiyo. Hivyo basi kama ikitokea mtu anataka kutumia spika za masikio ambazo zina waya itabidi aziunganishe kwa kupitia kebo spesheli ambayo itaunganishwa katika tundu la chaja katika iPhone 7. Usiwe na wasiwasi ni matumaini yangu kuwa kebo hiyo itakuja na simu

2. Spika Za Masikio Ambazo Hazina Waya

Airpods-Earphones mpya kutoka Apple

Airpods-Earphones mpya kutoka Apple

Jina la kimombo wanaziita ‘Wireless Headphones’ na hizi hufanya kazi bila hata ya kuwa na waya katika kifaa ili mradi tuu kuwe na njia nyingine ambayo inatumika kuunganisha vifaa hivyo viwili. Hili jambo mara ya kwanza wengi walizani ni utani au ni fununu tuu lakini imeonekana kuwa kampuni halina masihara kabisa juu ya jambo hili. Tulishazoa zile spika za masikio kutoka kwa Apple maarufu kama ‘Earpods’ lakini hizi zinaenda kwa jina la ‘Airpods’. Hapa usichanganyikiwe kwani ‘Airpods’ ni ‘Earpods’ ambazo hazina nyaya. Spika hizi zina uwezo wa kuunganika katika simu kwa haraka zaidi kuliko kile kitendo cha ku ‘pair’ katika Bluetooth.

INAYOHUSIANA  Thamani ya kampuni ya Apple imepanda

3. Kitufe Cha ‘Home’ Hakibonyezeki Tena

Kitufe Cha Nyumbani (Home) Katika iPhone

Moja kati ya vitu vikubwa sana vinavyoitambulisha simu ya iPhone ni kile kitufe chake cha kurudi nyumbani (home) katika skrini ya simu. Kitufe hichi hakijatolewa ila kwa sasa kimefanyiwa mabadiliko. Kwa kifupi ni kwamba kitufe hicho kitakuwa hakibonyezeki ila kitakuwa ni cha kutachi (touch). Bado kitufe hichi kipya kinatarajiwa kuleta majibu sawa na kile cha mwanzo na pia inategemewa yakawa hata ni zaidi.

4. Kamera Mbili

iPhone 7 Plus Ikiwa Na Kamera Mbili Wakati 7 Ikiwa Na Kamera Moja

Toleo kubwa la simu za iPhone 7 (Yaani iPhone 7 Plus) linakuja na kamera mbili kwa nyuma. Usishtuke! Kamera hizo ni kwamba kila moja itakuwa na kazi yake spesheli. Kwa haraka haraka ni kwamba kamera moja itakuwa na uwezo wa kuchukua picha katika eneo kubwa na nyingine katika eneo dogo.

Pia uwezo wa kuvuta picha kwa karibu wa kamera hizo unatofautiana. Kamera katika iPhone 7 ya kawaida inaweza ukapiga picha katika eneo kubwa na maboresho mengine mengi katika kamera kutoka katika simu ya iPhone 6s.

INAYOHUSIANA  Apple wafanya iwe vigumu zaidi ku'hack iPhone kwa Kuzima Uwezo wa USB

5. Toleo La Pili La Saa Janja Kwa Apple

Saa Janja Mpya Kutoka Apple

Apple wametoa kizazi cha pili cha saa zake janja, kwa sasa saa hii inajulikana kama ‘Apple Watch Series 2’. Saa janja hii ina sifa za aina yake na maboresho mengi kulinganisha na saa yake ya zamani. Kwa mfano saa hii inakuja na kioo cheupe – mara mbili — zaidi ya kioo cha saa iliyopita. Prosesa yake imebadilishwa, Apple wanasema kuwa saa hii itakuwa na ufanisi wa asilimia 50 zaidi ya saa iliyopita. Ukiachana na hayo, pia muonekano wake umeboreshwa.

Mambo Mengine Ni Pamoja Na :- 

– Saa janja mpya inakuwa na uwezo wa kutoingia maji mpaka kufikia kina cha 50m (nzuri sana kwa wale wanao ogelea). Pia inakuja na uwezo wa GPS na hii itakuwa ni msaada mkubwa kwa wale watu wanaofanya mazoezi.

– Mchezo wa Pokemon Go utakuwa unapatikana pia katika saa janja hizo.

– iOS 10 inatoka tarehe 13 mwezi huu (9). Na inakuja na mambo mengi sana, Ingia hapa kuyajua baadhi.

– OS mpya ya Mac yaani ‘macOS Sierra’ itatoka tarehe 20 mwezi huu (9).

Nini nimesahau? Hebu nikumbushe hapo chini sehemu ya comment. Ningependa kusikia kutoka kwako.

Kumbuka kutembelea mtandao wako pendwa wa TeknoKona ila siku ili kujipatia habari na maujajna ya teknolojia. Kumbuka TeknoKona Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa Teknokona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com