Yanayojulikana Kuhusiana Na Samsung Galaxy Note 8 Mpaka Sasa!

0
Sambaza

Janga ambalo lilitokea kwa kampuni ya Samsung kuhusiana na simu zake za Samsung Galaxy Note 7 limeipa pigo kubwa kampuni hilo.

Ukiachana na kampuni kusitisha kuzalisha na kuuza simu hizo baada ya kutokea kwa milipuko kadhaa ya simu hizo katika eneo la betri, bado kampuni imepoteza mabilioni ya dola za kimarekani.

Simu Za Samsung Galaxy Note 7

Simu Za Samsung Galaxy Note 7

Baada ya kampuni kuachana na simu hiyo simu inayotegemewa kuwa ya mbele katika matoleo hayo ni Samsung Galaxy Note 8 ambayo inatarajiwa kutoka mwaka 2017.

Siku Ya Simu Hii Kuingizwa Sokoni.

Ni jambo la wazi kabisa kuwa kampuni ya Samsung imejiwekea tabia ya kuanza kuuza rasmi simu zake zile za matolea ya Galaxy S (mfano S4, s5, s6 nk) kila ifikapo mwezi februari au machi. Na hata zile simu zake za matoleo ya Galaxy Note katika miezi ya agosti kila mwaka. Na inategemewa hata kwa mwaka 2017 watafuata utaratibu huo huo ambao tiyari umeshazoeleka kwa kiasi kikubwa sana.

SOMA PIA:  WhatsApp Katika Mchakato Wa Kuongeza Vipengele 2 Vikubwa!

Makampuni mengi ya kutengeneza na kuuza simu huwa yanakuwaga na miezi spesheli ya kuingiza bidhaa zake sokoni hata kampuni ya simu na kompyuta ya Apple nayo wembe ni ule ule (ina miezi spesheli za kuingiza bidhaa sokoni).

Lakini hili la Samsung Note 8 tuliangalie kwa jicho la tatu, maana kutokana na milipuko iliyotokea na kulichafua jina la Samsung Galaxy Note 7 inawezekana dhahiri simu hii (Samsung Note 8) ikawahi kutoka kuliko wengi wanavyotarajia au kuliko ilivyo zoeleka. Hivyo basi pengine mtu asishangae kuiona simu hii sokoni katika miezi ya kwanza kwanza kwa mwaka 2017.


Fununu Juu Ya Sifa Za Ndani Za Samsung Galaxy Note 8.

• Kioo cha inchi 5.7 na pia itakuwa inaruhusu teknolojia ya 4K
• Simu inaweza ikaja na ujazo wa RAM wa GB 6 au GB 8
• Prosesa yake inaweza ikawa Qualcomm Snapdragon 830
• Ujazo wake wa ndani wa memori ya kuhifadhia vitu unaweza ukafika hadi GB 256

SOMA PIA:  Kampuni ya Samsung yatajwa kuwa yenye thamani zaidi Korea Kusini miaka 7 mfululizo

Pia taarifa hizi sio rasmi sana kwani kampuni ya Samsung wao kama wao bado hawajatoa neno lolote kuhusiana na vitu gani vya kutegemewa katika simu hii ijayo
Punde tuu tukipata taarifa ambazo zinatoka katika vyanzo vya Samsung moja kwa moja tutakua wa kwanza kukujuza.

Pia kumbuka kikubwa ambacho kilisababisha madhara makubwa katika simu ya Samsung Galaxy Note 7 ni betri. Hivyo basi ni tumaini letu kuwa kampuni itatumia nguvu nyingi katika kuhakikisha kuwa inalifanyia kazi jambo hilo na kuja na kilicho bora zaidi kwa watumiaji wake.

Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini sehemu ya comment. Je na wewe unaisubiria kwa hamu? Au una simu nyingine katika kichwa chako?

SOMA PIA:  Mwanzilishi Wa Android Anakuja Na Simu Yake, Mei 2017! #Muendelezo

Tembelea TeknoKona kila siku kwa habari na maujanja mbalimbali yanayohusu teknolojia. Kumbuka TeknoKona Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa Teknokona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com