Ingawa katika nchi nyingi za Afrika bado watu wachache wanatumia sana baiskeli kama chombo kizuri cha usafiri hali ni tofauti sana katika nchi zilizoendelea. Wengi hasa wanafunzi na ata wafanyakazi huwa wanapendelea kutumia baiskeli na ata hawakudharau pale unapotumia usafiri huo ukilinganisha na hali ilivyo katika nchi zetu hasa mijini. Na hii inafanya biashara ya baiskeli kuwa ya faida sana katika nchi zilizoendelea.
Kutokana na utumiaji mkubwa wa baiskeli katika nchi nyingi kama vile Marekani na nyingi za barani ulaya kumekuwa kunatokea na wizi mwingi wa baiskeli pale ambapo utaiweka (park) pale unapoingia ofisini, chuo n.k. Jambo hili limewasukuma vijana watatu nchini Marekani kuungana na kuja na teknolojia ya hali ya juu kwenye utengenezaji wa baiskeli ambayo hamna jinsi ya kuiiba bila kuiaribu kabisa. Yaani ukifanikiwa kuiiba basi utakuwa ushaivunja vunja na ni kazi itakayokuwa imechukua muda mrefu sana kiasi cha kuweza kukamatwa.
Badala ya kutumia mnyororo n.k utaweza kutumia vifaa vya hiyo hiyo baiskeli kuweza kutengeneza kufuli na ukabana kwenye chuma au mti wa karibu.
Baiskeli hizo zilizopewa jina la ‘The Unstealable Bike’, yaani baiskeli isiyoibika, moja inauzwa kwa takribani milioni 1 ya kitanzania ($500). Jina rasmi likiwa ni YERKA. Kupitia teknolojia mbalimbali wameweza kutengeneza vyuma kazaa katika viunganishi vya baiskeli kuvifanya viweze kuchomolewa na kutengeneza komeo (lock) pale unapotaka kuiacha mahali, yaani badala ya kutumia mnyororo n.k utaweza kutumia vifaa vya hiyo hiyo baiskeli kuweza kutengeneza kufuli na ukabana kwenye chuma au mti wa karibu.
Pia kupitia teknolojia ya nati spesheli ambayo wewe tu ndio unakitu cha kufungulia ambacho hakifanani na zingine wameweza kufanya ata utoaji wa matairi kuwa mgumu zaidi na hivyo kuwazuia wezi kabisa kufanya wizi wa matairi ya baiskeli yako.
Pia kama mteja ataongeza takribani laki 3 atapewa baiskeli hii ikiwa na teknolojia ya kukuwezesha kupata taarifu za baiskeli kupitia kwenye app ya Android au iOS.
Vijana watu waliokuwa chuo ndio walikuja na wazo la utengenezaji wa baiskeli hii, vijana hao baada ya kupata mtaji mdogo wa kuanzia walisimamisha masomo yao chuo na kujikita katika utengenezaji wa kampuni yao mpya. Vijana hao ni Cristóbal Cabello – ana miaka 22, Andrés Roi Eggers, – ana miaka 23 na Juan José Monsalve, – ana miaka 24.
Je, wewe unaweza kutumia takribani dola 500 za Marekani (Tsh Milioni 1) kwa ajili ya kununua baiskeli? Teknolojia ndio hiyo inazidi kukua labda siku moja tunaweza kuziona baiskeli hizi hadi huku kwetu, kwa sasa unaweza kuzipata kwa kuchangia mtaji unaowezesha utengenezaji wa baiskeli hiyo kwenye mtandao wa IndieGogo – https://www.indiegogo.com/projects/yerka-the-unstealable-bike
Soma Pia – Je Unaifahamu Teknolojia ya Viti Visivyo na ‘Miguu’?
No Comment! Be the first one.