Youtube kuleta uwezo wa kuwa mubashara kwenye Android - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Youtube kuleta uwezo wa kuwa mubashara kwenye Android

0
Sambaza

Mubashara (live stream) ni teknolojia ambayo inatokea kupendwa na wengi kutokana na ule uwezo wa kuonyesha watu kile ambacho mhusika anakifanya kwa wakati huo kupitia picha jongefu.

Siunafahamu ya kuwa unaweza kurusha picha ya mnato ukiwa mubashara kwenye Facebook, Instagram na hata Twitter? Basi nao Youtube hapo njiani kuleta kitu kama hicho kwa watumiaji wa simu rununu zenye kutumia mfumo endeshi wa Android; enter site yaani kupitia kamera ya simu yako kupitia Youtube ukaanza kurusha video mubashara na watu wakaona kinachoendelea.

Asus, LG, Motorola, Nokia na Samsung ni simu ambazo zinatarajiwa kuwa na uwezo wa kuruhusu mtumiaji kwenda mubashara kwenye Youtube.

Je, uwezo wa kwenda mubashara kwenye Youtube kupitia simu ni kitu kipya?

La hasha! Si kitu kipya kabisa kwani kama mtu ni mtu ambaye anapenda kuijua simu yake vyema basi atakuwa anajua kuwa http://directadvantagellc.com/master-produce-list/ Sony Xperia Z3 tangu mwaka 2014 simu hizo zina uwezo wa kwenda mubashara kwenye Youbute. Halikadhalika, watch Samsung Note 5 iliyotoka mwaka 2015 pia inaruhusu mtumiaji kwenda mubashara kwenye Youtube.

kuwa mubashara kwenye Android

Kwenda mubashara kwenye Youtube: Katika mpango wa kuwezesha simu janja kuwa na uwezo wa kwenda mubashara kwenye Youtube ni zile ambazo zinatumia Android Marshmallow (API 23) na kuendelea.

Wanaoingia Youtube kupitia kompyuta hawajasaaulika

Kupitia kompyuta Youtube wamerahisisha na kuja na njia rahisi ambayo inamuwezesha yule anayetembelaea Youtube kupitia kommpyuta basi kuweza kwenda mubashara bila kupita njia ndefu; ukitembelea youtube.com/webcam utaweza kufuata hatua fupi na rahisi ili kwenda mubashara ila tu lazima kamera iwepo.

kuwa mubashara kwenye Android

Kwenda mubashara kwenye Youtube: Moja ya hatua za mwanzo kabisa kuweza kufanya kwenda mubashara kwenye Youtube kupitia kompyuta.

Je, kitu hiki ambacho Youtube wapo mbioni kukileta kwenye simu za Android kitaongeza wingi wa video na muda ambao watu wanatumia kuperuzi Youtube na pengine kuwa tishio kwa Facebook, Instagram na wengineo?

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Apple kufanyia matengenezo bidhaa zao bure
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.