Youtube Wazindua Huduma Ya 'Live Stream' Kwenye App Ya Simu Kwa Majina Makubwa! - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Youtube Wazindua Huduma Ya ‘Live Stream’ Kwenye App Ya Simu Kwa Majina Makubwa!

0
Sambaza

Mtandao wa kijamii wa Youtube ambao unajihusisha na maswala ya video ambao pia unamilikiwa na kampuni ya Google umeweka wazi kuwa umeanzisha huduma ya ‘Live Stream’

http://ohanama.com/free-trial-class

http://doinkdesign.com/2014/06/ Huduma hiyo kwa sasa ni kwa wale watu wenye majina makubwa kama vile Wasanii na wanasiasa. Hapo baadae kila mtu atapata nafasi ya kuitumia huduma hii kwa Youtube wana mpango wa kuhakikisha kuwa kila mtu anaifurahia hii huduma.

App Ya Youtbe Katika Simu

http://bitcoinsgreece.com/tag/bitcoin/ App Ya Youtbe Katika Simu

Huduma hii kutoka Youtube itakuwa ikiminyana vikali na huduma kama vile Facebook Live kutoka Facebook na Periscope Kutoka Twitter.

Lakini pia kumbuka Youtube ni kampuni ambayo imebobea sana katika maswala ya video hivyo basi hii inaweza ikawafanya wasipate changamoto kubwa sana na ya kutishia kutoka kwa makampuni mengine yanayotoa huduma ambayo inafanana na  hii

INAYOHUSIANA  Youtube: Kipengele cha Dark Mode kwenye simu


Kwa kuwa huduma hii inapatikana katika App ya Youtube katika simu basi hata muonekano wake utakuwa unafanana kabisa na video zingine za mtandao huu. Ukitaka kutafuta video utaweza kuitafuta kwa kawaida tuu kwa kuiandika katika kiboksi cha kutafuta (search) au ukaiona katika mapendekezo (recommended)

Siku hizi Video zinanachukua sehemu kubwa sana, App nyingi zinajikita sana katika kuhakikisha zinakuwa na kipengele cha video. App kama Snapchat imepata umaarufu kwa video zake fupi ambazo zinapotea mara tuu unapoziangalia au kwa masaa 24


Kwa Youtube hili nalo ni jambo zuri licha ya kwamba litawaongezea mapato lakini pia wanarahishisha namna ya mawasiliano baina ya watu na watu.

INAYOHUSIANA  Ifanye akaunti yako ya YouTube ikuingizie pesa

Niandikie hapo chini sehemu ya comment je wewe unaona ni vyema Youtube kuendelea na hili zoezi lao au wabakie tuu na huduma ya video ambayo sisi tumeizoea?

Kwa habari za moto kama hizi na zingine za moto zaidi tembelea mtandao wako pendwa wa TeknoKona kila siku. Kumbuka TeknoKona Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa Teknokona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comments are closed.