YouTube yafanya mabadiiko ya logo. Huu ni muendelezo wa maboresho mbalimbali ambayo YouTube imekuwa ikiyafanya ili kuboresha huduma zake kwa watumiaji wake wa kompyuta na simu janja.
Mabadiliko hayo yana siku chache ambapo yanahusisha logo na mpangilio wa video na muonekano wa matangazo.
Mabadiliko ya logo ya YouTube yashafanyika mara kadhaa lakini kwa sasa ndio yatakuwa mabadiliko makubwa. Muonekano wa logo wa sasa kumewekwa alama ya batani ya kucheza (Play).
YouTube yafanya mabadiiko ya logo.
Muonekano wa Logo yake ya zamani ni ule wa neno lake la ‘Tube’ kuwa ndani ya kiboksi kilichokuwa kinawakilisha muonekano wa TV, kwa sasa kiboksi hicho kitajitegemea na kitakuwa nje ya neno ‘YouTube’.
Mabadiliko haya ya YouTube yamezingatia kuifanya kuwa na wepesi zaidi pale mtu anapofungua kurasa za YouTube. Hasa hasa kwa watumiaji wa simu za mkononi.
Mabadiliko hayo tayari yapo kwenye kompyuta na Simu yakiendelea kadri yalivyopangwa. Mabadiliko hayo yamepokelewa kwa hisia tofauti na watumiaji wa YouTube. Wapo waliofurahi mabadiliko hayo na kusema yapo safi.
Lakini wapo walioponda na kusema ni bora ungebaki muonekano ule wa awali kwani ulikuwa mzuri zaidi kuliko wa sasa.