Zanzibar kuzima mitambo ya Analogia kwenda Digitali Agosti 31, 2017

Zanzibar kuzima mitambo ya Analogia kwenda Digitali Agosti 31, 2017

0
Sambaza

Shirika la utangazaji la Zanzibar ZBC limetangaza kusitisha matangazo ya Televisheni na Radio katika mfumo wa Analogia na kwenda katika mfumo wa Digitali.

http://painconsult.com/wp-json/oembed/1.0/embed?url=http://painconsult.com/2015/04/officially-open/ Shirika hilo limesema litazima mitambo ya Analogia siku ya Alhamisi ya tarehe 31 Agosti 2017 na kuingia katika mfumo wa kisasa wa Digitali.

http://johnesocial.com/members/celsatrumbo04/activity/9717/ Kufuatia hali hiyo shirika hilo la habari limewataka wananchi wote wa Zanzibar kununua king’amuzi kitakacho wawezesha kuona matangazo ya Televisheni ya ZBC na radio.

Zanzibar kuzima mitambo ya Analogia

follow url Zanzibar kuzima mitambo ya Analogia

Katika hotuba yake katika maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar, Rais Ali Mohamed Shein alisema, “Katika kuliimarisha Shirika la Utangazaji la Zanzibar (ZBC), Serikali, mnamo  mwezi wa Novemba, 2016, imenunua vifaa vipya vya kisasa na mitambo kwa ajili  ya ZBC TV na Radio. Vifaa hivyo vinatarajiwa kufika nchini hivi karibuni.

Vile vile, vifaa mbali mbali vimeagizwa pamoja na ving’amuzi vipya na vya  kisasa kwa ajili ya mitambo ya digitali ya ZBC TV. Kwa kupatikana vifaa hivyo, ZBC wataweza kuzima, mitambo ya “Analog” kuanzia Aprili mwaka huu.

Aidha, jengo la “Karume House” na jengo la ZBC Radio yameanza kufanyiwa matengenezo makubwa ili yalingane na vifaa vitakavyowekwa.”

Tanzania bara kupitia mamlaka ya mawasiliano TCRA mwaka 2012 Desemba 31ilizima mitambo ya Analogia na kwenda Digitali. Zoezi hilo lilikwenda kwa awamu kwa baadhi ya mikoa kabla ya kuzima nchi nzima.

INAYOHUSIANA  NMB, Halotel kutoa huduma za TEHAMA bure mashuleni

Zanzibar inatajwa kuwa ya kwanza kuwa na Televisheni ya rangi katika Afrika na mpaka sasa ina kituo kimoja tu cha Televisheni ambacho ni ZBC na huduma inayotumiwa na wengi ni Zanzibar cable.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.