HTC watambulisha Simu mpya; Zifahamu simu za HTC Desire 10

HTC watambulisha Simu mpya; Zifahamu simu za HTC Desire 10

0
Sambaza

HTC watambulisha simu mbili za familia ya Desire 10. Simu hizo ni HTC Desire 10 Lifestyle ambayo tayari inaingia sokoni wakati Desire 10 Pro itaanza kupatikana mwezi ujao (Oktoba).

enter htc desire simu

HTC Desire 10 Pro

buy finast walgreens Hii ndiyo iliyo na sifa za uwezo wa juu (specs). Inakuja na kioo cha ukubwa wa inchi 5.5 FullHD IPS Display, kikiwa na teknolojia ya Gorilla Glass.

HTC Desire 10 Pro

Muonekano wa HTC Desire 10 Pro

Sifa zaidi;

 • RAM ya GB 4/3, diski uhifadhi wa GB 64/32 (unaweza tumia MicroSD)
 • Prosesa ya hadhi ya juu ya Mediatek Helio P10
 • Kamera ya Megapixel 20 (lesar autofocus, dual-LED flash)

  htc desire 10

  Muonekano wa nyuma wa HTC Desire 10 Pro, ukionesha kamera na flash mbili.

 • Kamera kwa ajili ya selfi inakuja na Megapixel 13 na uwezo wa picha za selfi za panorama za nyuzi 150 kwa ajili ya selfi zinazohusisha kundi kubwa la watu.
 • Inakuja na teknolojia za kimawasiliano za 2G, 3G na 4G LTE, WiFi, Bluetooth, NFS
 • Nyuma yake ina eneo kwa ajili ya sensa za miguso (fingerprint sensor). Kwa kutumia eneo hilo utaweza ku’unlock simu na ata pia ku’control kamera pale unapopiga picha
 • Suala la teknolojia ya kuchaji inakuja na iliyozoeleka ya MicroUSB
 • Ukubwa mm 156.5 x 76 x 7.9, na uzito wa gramu 165
 • Betri, mAh 3,000

HTC Desire 10 Lifestyle

Hii inakuja na sifa za kawaida kidogo na hivyo inalenga zaidi sifa za sifa ya kati. 

Muonekano wa HTC Desire 10 Lifestyle

Kiukubwa haina tofauti sana na Desire 10 Pro, ina kioo cha ukubwa wa inchi 5.5 ila badala ya kuwa na sifa ya FullHD hii inakuja na HD ya kiwango cha kawaida. 720p.

Sifa zinginezo;

 • Kutakuwa na order proscar uk matoleo mawili ya Desire 10 Lifestyle, kuna la RAM ya GB 3 na diski uhifadhi wa GB 32. Toleo jingine la RAM ya GB 2 na diski uhifadhi ya GB 16, zote zitakuwa na eneo la microSD. Tofauti zitakuwa ni bei.
 • Prosesa ya Snapdragon 400 (hii ni ya kawaida sana)
 • Kamera; Megapixel 13, ya selfi megapixel 5.
 • Nayo inakuja na teknolojia za 2G, 3G na 4G LTE
 • WiFi, Bluetooth, NFC, headphone jack na microUSB.
 • Ukubwa mm 156.9 x 76.9 x 7.7, inakaribiana kulingana sawa tuu na HTC Pro. Ila ni nyepesi kidogo, inauzito wa gramu 155
 • Betri, mAh 2,700

Simu zote mbili zitakuja katika rangi mbalimbali kama vile; nyeupe, bluu, nyeusi – (Stone Black, Polar White, Royal Blue na Valentina Flux). Katika simu za rangi zote kutakuwa na mstari wa rangi ya dhahabu pembezoni na nyuma.

HTC Desire  10 Lifestyle inapatikana kwa bei ya kuanzia takribani dola 324 za kimarekani | Tsh 700,000 | Ksh 32,800. Bei ya toleo la Desire 10 Pro bado haijatolewa. Vipi, unazionaje simu hizi? Tuambie kwenye comment.

Vyanzo: GSMArena na mitandao mbalimbali

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  iPhone mpya yenye laini mbili kuuzwa Uchina tu!
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.