Zijue emoji mpya zinazokuja 2017

0
Sambaza

Katika uandishi kwenye mitandao ya kijamii emoji zinachukua nafasi kubwa hasa katika kunogesha mazungumzo, kila mwaka muungano wa Unicode (ambao ndio unaamua emoji gani zitumike) hukaa na kuamua waongeze emoji mpya zipi katika orodha ya emoji.

Mwaka huu muungano huu umekwisha kaa na tayari umetoa mapendekezo ya emoji mpya kwaajiri  ya mwaka 2017.

emoji mpya

Baadhi ya emoji mpya

Unicode wamependekeza emoji 51 ambazo bado zilikuwa hazipo katika matoleo yaliyopita, emoji hizi kama zitapita basi zitaanza kutumika mwakani. Ni bado mapema saana kujua kama emoji zilizopendekezwa ndio zitakazopitishwa kuna uwezekano yakafanyika mabadiliko kadhaa.

SOMA PIA:  LG V30: Simu janja iliyobora kuleta ushindani kwa Samsung na Apple

Kwa watumiaji wa android basi watakaozipata ni wale tu ambao watakuwa wanatumia vifaa ambavyo vitakuwa na OS zilizotoka baada ya toleo hili la emoji lakini kwa wale ambao wanatumi iOS basi wao watazipata emoji hizi baada ya kuanza kutumia toleo jipya la iOS.

emoji mpya

Emoji pendekezwa za chakula

Katika pendekezo la emoji hizi mpya baadhi ya emoji zilizopo ni pamoja na emoji ya Hijab, mwanamke aliyevaa hijab, mwanaume aliyefuga ndevu nyingi, kichwa cha twiga na nyinginezo nyingi.

SOMA PIA:  Wafariki wakipiga picha ya 'selfie' mbele ya treni

Unicode wanajaribu kuzidi kuwa na emoji ambazo zinawakilisha vitu vingi zaidi ili waweze kuwavutia watumiaji wa mitandao kutumia zaidi emoji hizo. Kwa upande mwingine hii ni habari nzuri kwa wanaharakati ambao wamekuwa wanapigania saana usawa katika uwakilishi wa emoji hizi.

Tuambie je ipi kati ya emoji hizi ambazo zinakuja unadhani utaitumia zaidi zikiwa zinapatikana..

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com