Zima "Automatic updates" kwenye simu yako - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Zima “Automatic updates” kwenye simu yako

0
Sambaza

Jambo la simu kufanya masasisho ya apps (programu tumishi) bila ridhaa yako ni jambo linalowakera wengi hasa ukizingatia kuwa wakati simu inafanya masasisho MB’s huenda kwa kasi sana.

Kufanya masasisho ya programu tumishi zilizopo kwenye simu yako ni jambo muhimu ili kuweza kupata mambo mapya yaliyoboreshwa kwenye app husika. Fuatilia kwa makini makala hii ili uweze kuondokana kadhia hii inayomaliza MB’s kwa matumizi ambayo hukuyatarajia kwa wakati huo.

Jinsi ya kuzima masasisho kwenye simu za Android.

Kwa simu za Android ambazo ndio zinatumiwa na wengi sana kutokana na bei zake kuwa nafuu kulinganisha na zile zinazotengenezwa na Apple. Ili kuweza kuzima ‘automatic updates‘ basi fungua http://amidwifeonthepath.com/obstetric-violence/ Google Play>> go to link Settings>> follow url Auto update apps.

Ukishafungua Google Play, bofya upande wa kushoto juu ili kuweza kupata settings na kisha kuendelea na hatua itakayofuata.

Mahali husika patakapokuwezesha kuzima/kuwasha masasisho (updates).

Kwenye ukurasa wa Auto update apps utaweza kuchagua iwapo unataka simu yako isipate masasisho kabisa au ipate masasisho iwapo tu inapata intateti kupitia WIFI au iendelee kuweka masasisho bila ya mtumiaji kupenda.

INAYOHUSIANA  Piga simu kwa watu wengi kwa njia ya WhatsApp

Jinsi ya kuzima masasisho kwenye iPhone/iPad.

Mbinu ya kuzima automatic update hatofautiani sana na ile ya kwenye simu zinazotumia programu endeshaji ya Android. Hivyo ni suala la kwenda kwenye Settings >>iTunes & App Store>>Updates. Kisha rudisha nyuma kuelekea kushoto ili kuiamuru simu yako kutofanya masasisho bila wewe kutaka.

Unaweza ukaiamuru simu/iPad kuweka masasisho kwa kutumia MB’s ulizonazo.

Masasisho ni muhimu sana hasa kwa zile apps ambazo unazitumia mara kwa mara; TeknoKona tunashauri kuondoa zile apps ambazo hazina umuhimu kwako na kubaki na zile zenye umuhimu tu.

Vyanzo: Gadgets360, mitandao mbalimbali.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.