ZoomTanzania Yaboresha Soko La Biashara Mtandaoni! - TeknoKona Teknolojia Tanzania

ZoomTanzania Yaboresha Soko La Biashara Mtandaoni!

0
Sambaza

ZoomTanzania ni mtandao (namba moja?) ambao unajihusisha na kuuza na kununa bidhaa mtandaoni pamoja na mambo mengine mengi kama vile kutafuta ajira  katika mtandao n.k.

buy inderal 10mg

Lamictal available canada Kuna mengi sana ambayo yamebooreshwa mpaka sasa na kama wewe ni moja kati yawafuatiliaji wazuri wa mtandao huo wa ZoomTanzania utakuwa tayari umeshaona baadhi. Moja kati ya mabadiliko hayo ni pamoja na Logo yake mpya bila ya kusahau kuwa kwa sasa tovuti hiyo inapatikana mpaka kwa buy finasteride original lugha ya kiswahili.

Muonekano Mpya Wa Mtandao Wa ZoomTanzania

Muonekano Mpya Wa Mtandao Wa ZoomTanzania

ZoomTanzania imeboresha mambo mengi sana ili kuhakikisha kuwa inatoa huduma bora kwa wateja wake katika mtandao huo. Tovuti hii kwa sasa utaifaidi vizuri pia kama unatumia simu janja (smart phone) yako.

“Kwa kuwa zaidi ya asilimia 67 ya Watanzania wanatumia simu za mkononi ambazo nyingi ni ‘smart – phones’ kuuza au kununua bidhaa na huduma nyinginezo kupitia tovuti ya ZoomTanzania.com, tovuti hii itawarahisishia zaidi kwa kuwa imefanyiwa mabadiliko makubwa. Zoom ni tovuti ambayo iliwezeshwa kwa ajili ya simu ndogo za mkononi pekee (feature phones). Baada ya kugundua kuwa watumiaji wengi wa simu hutumia ‘smartphones’, tukauongezea uwezo mfumo wa ZoomTanzania ili kurahisisha watumiaji kuweka bidhaa zao katika tovuti kiurahisi zaidi na pia kuwasiliana na muuzaji kiurahisi zaidi,” – Alisema mtaalamu wa tovuti ya ZoomTanzania, Terence Silonda

Kumbuka zaidi ya asilimia 67 ya watanzania wanatumia simu  na wengi kati ya hao wanatumia simu janja. vile vile wengi kati ya hao wanazitumia simu janja zao katika kuuza na kununua vitu kupitia mtandao na ZoomTanzania ndio mahali sahihi pa kufanya hayo yote.

INAYOHUSIANA  Waliopewa dhamana ya kusimamia mifumo ya TEHAMA serikalini waonywa na kutakiwa kuzingatia weledi kazini

Ni wazi kwamba kwa mara ya kwanza kabisa mtandao huo ulikua umetengenezwa spesheli kwa zile simu ambazo sio janja (simu jinga?) au kwa lugha ya kimombo wanaita  feature phone.

Pia maboresho mengine katika mtandao kwa sasa ni kuongezeka kwa machaguo mengi wakati mtumiaji anatafuta vitu, ukubwa wa maandishi umeongezwa ili kuhakikisha kila mtu anayaona vyema maandishi na maboresho mengine mengi.

ZoomTanzania ni tovuti inayoongoza Tanzania kwa matangazo ya biashara kupitia mtandao. Inahusisha biashara 7,500, watumiaji waliosajiliwa zaidi ya 200,000 na ikiwa inatembelewa hadi mara 40,000 kwa wastani wa siku. Ni tovuti inayoaminika zaidi katika kuunganisha wanunuzi na wauzaji nchini Tanzania.
Muonekano Mpya Wa Mtandao Wa ZoomTanzania

Muonekano Mpya Wa Mtandao Wa ZoomTanzania

Tovuti hii ilibuniwa spesheli kwa ajili ya soko la Tanzania na uzinduzi huu ni mwanzo tuu wa mambo  mengi yanayokuja kutoka ZoomTanzania. Maboresho hayo ya baade ni kama upanuzi wa wigo wa mtandoa huo na kuwaunganisha wauzaji na wanunuzi wa bidhaa mbalimbali.

INAYOHUSIANA  Waliopewa dhamana ya kusimamia mifumo ya TEHAMA serikalini waonywa na kutakiwa kuzingatia weledi kazini

Www.ZoomTanzania.Com

Tuambie wewe umelipokea hili vipi kumbuka ZoomTanzania ni mtandao ambao upo hapa nchini Tanzania. Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini sehemu ya comment

Kumbuka kusambaza makala na pia kuungana nasi kupitia Facebook, Twitter, Instagram, YouTubeTelegram na Google Plus

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa Teknokona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comments are closed.