‘Privacy’- Mark Zuckerberg wa Facebook afunika Kamera na Mic ya Laptop Yake

1
Sambaza

Suala la usalama wa data na kuchunguzwa na vifaa vyetu ni jambo linalozungumzwa sana. Na kuonesha ni jinsi gani suala hili ni nyeti laptop ya mwanzilishi na mkurugenzi mkuu wa Facebook, Bwana Mark Zuckerberg, imeonekana ikiwa imezibwa kamera na kinasa sauti – Mic.

Katika picha yake ya kusheherekea mafanikio ya Instagram kufikisha idadi ya watumiaji milioni 500 aliyopigwa akiwa kwenye meza yake ofisini watu wajanja wamefanikiwa kuchunguza laptop iliyomezani kwake na kuthibitisha ya kwamba laptop hiyo imezibwa sehemu hizo.

SOMA PIA:  Usalama wa nywila kwenye simu yako unatokana na ushikaji wa simu

Zack facebook afunika kamera

Vitu vitatu vilivyoonekana kwenye laptop yake;

  • Kamera (webcam) imezibwa
  • Sehemu ya Kinasa sauti (Mic) imezibwa pia
  • Anatumia programu ya Thunderbird kwa ajili ya kusoma na kutuma barua pepe

Picha hiyo baada ya ‘kuzoom’, angalia maeneo yaliyozungushiwa rangi nyekundu..

Kumeshakuwa na taarifa zinazoonesha ukuaji wa udukuzi unaohusisha mtu aliyembali na wewe kuvamia kompyuta ya mtu kwa kutumia intaneti na kisha kuendesha programu za kompyuta husika, hii ikiwa ni pamoja na kuwasha kamera na kupiga picha au kurekodi video na kisha kutuma kwa mdukuzi huyo.

SOMA PIA:  Marekani: Programu ya Antivirus ya Kaspersky Lab marufuku serikalini

Kwa kiasi kikubwa inaonekana mwenyewe hakugundua kama picha hiyo ingeoonesha jambo hilo. Pia tayari Facebook imeshashutumiwa ya kwamba inatabia ya kuchunguza watu kupitia app yao ya simu ambayo pale unapoipakua huwa inapewa uwezo wa kuwasha na kutumia kamera na kinasa sauti.

Kwa mmoja wa vijana matajiri zaidi duniani ana haki zote za kuwa na wasiwasi juu ya kushambuliwa kimtandao – kupigwa picha akiwa chumbani n.k ? ? ? ?

Unamtazamo gani na suala hili?

 

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com