fbpx
Intaneti, Tanzania, Teknolojia

Fahamu Tofauti Kuu Kati ya Teknolojia za 2G, 3G, 4G n.k

fahamu-tofauti-kuu-kati-ya-teknolojia-za-2g-3g-4g-n-k

Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163
Sambaza

Simu, imekuwa imekuwa zaidi ya simu katika miaka hii. Miaka ya zamani simu ilikuwa ni simu ikimaanisha inakupa uwezo wa kupiga na kupokea simu tuu. NDIYO! Yaani ata suala la ujumbe mfupi lilikuja baadae, ata uwezo wa kutosha mfukoni mwako lilikuja baadae. Kwa miaka hii tuna simu, simu za kawaida (featured phones) na tuna hadi simu-janja (smartphones).

Katika kipindi cha miaka 10-20 hivi nyuma kifaa hichi kimepitia mabadiliko makubwa kutoka kuwa na uwezo wa kufanya kazi moja hadi kufikia sasa ambapo simu-janja inauwezo wa kufanya kazi mbalimbali nje ya kupiga na kupokea simu tuu. (Soma Makala Yetu – Tumia Simu Yako Kama Vifaa 10 Tofauti Vya Ki-elektroniki!  )

Katika mabadiliko yote haya eneo la huduma ya intaneti limechangia kwa kiasi kikubwa sana kuwezesha mafanikio mengi katika kuwezesha mambo mengi sana kuweza kufanyika katika simu. Kuanzia miaka ile ya GPRS – kisha tukaanza kuona EDGE kwenye simu zetu..3G, leo fahamu maana zake na tofauti zake.

Kwa kuanzia fahamu ya kwamba G – inasimama kumaanisha ‘Generation’, hapa inatumika kama kuelezea teknolojia ya miaka/kipindi flani. Na hili teknolojia husika ya intaneti hikidhi kuwa katika kundi husika, yaani mfano 3G na 4G basi lazima ifikie viwango flani vilivyoweka kwa kundi husika. Viwango hivi vinatolewa na shirika la umoja wa mataifa linalohusika na masuala ya teknolojia za kimawasiliano, na kigezo kikubwa zaidi ni suala la kasi yake katika kuhamisha data (intaneti).

1G ni simu za kizazi cha kwanza kabisa katika teknolojia ya mawasiliano katika mfumo wa bila waya (wireless). Wakati huu ndio simu za mkononi (zikiwa kubwa kwelikweli enzi hizo) zilianza kutengenezwa na kununuliwa. Hii ilikuwa katika miaka ya 1980, na moja ya simu maarufu enzi hizo kuanza ni Motorola DynaTAC. Hakukuwa na huduma ya intaneti katika mfumo huu wa teknolojia. Kulikuwa na modemu kwa ajili ya intaneti kwa ajili ya kutumika kwenye kompyuta, ila zilikuwa zinatumia teknolojia ya ‘Dial up’, yaani kwenye mipangilio (settings) unakuwa kama unapiga simu hivi ndio unakuwa unaunganishwa katika huduma ya intaneti. Na gharama ilikuwa unalipia kulingana na muda ambao umekuwa umeunganishwa kwenye intaneti, yaani kama vile dakika za maongezi.

Kuja na uwezo wa kujiunga mara zote bila ata ya kutumia teknolojia ya Dial Up ndio kulizaa teknolojia ya 2G kwa kuanzia na GPRS.

Teknolojia za 2G;

GPRS

GPRS ndiyo teknolojia ya kwanza kwenye simu iliyoleta uwezo wa kutumia data, yaani intaneti. Teknolojia hii ipo katika familia ya teknolojia za 2G, yaani ‘2nd Generation’. Kirefu cha GPRS ni ‘General Packet Radio Service’, kiasi kikubwa zaidi cha kasi ya intaneti ndani ya teknolojia hii ni hadi kufikia kati ya kb 35 hadi 171 kwa sekunde. Lakini mara nyingi huwa chini ya hapo.

INAYOHUSIANA  Fahamu Matoleo Rasmi ya Windows 10

Katika kutumia teknolojia hii ndio utaweza kufungua mtandao wowote au ata kutuma barua pepe kwenye simu yako, tatizo ni moja tuu..itachukua muda mrefu sana mtandao kufunguka au ata hiyo barua pepe kwenda.

Hapa mfano wa kasi yake ni kama vile mwendo wa kutembea kwa miguu..

EDGE

Kibongo bongo, yaani Tanzania utakuwa umeona sana alama ya E au EDGE ikiwa imekamilika katika simu yako. Ukiona E, ujue ni EDGE na kirefu chake kimombo ni ‘Enhanced Data rates for GSM Evolution). Kwa kiasi kikubwa teknolojia hii ilitengenezwa kama maboresho ya teknolojia ya GPRS, hapa uwezo uliongezwa zaidi katika suala la kasi ya uhamishaji wa data katika huduma ya intaneti.

Teknolojia hii huwa inategemewa kuweza kuwa na kasi ya hadi kufikia kb 120 hadi 384 kwa sekunde, lakini mara nyingi huwa chini ya hapo. Teknolojia hii ipo juu zaidi ya GPRS lakini ni ya chini sana ukilinganisha na 3G. Wataalamu wengine huwa wanaiona EDGE kama ni 2.5G au 2.75G kutokana na kuwa kasi zaidi ya GPRS.

Hapa mfano wa kasi yake tunaweza fananisha na kamwendo ka kwenda kwa baiskeli. Unajitahidi kidogo ila si kasi sana.

3G – pia HSPA n.k

Teknolojia ya 3G ilitengenezwa kwa ajili ya kutoa maboresho mapya ukilinganisha na teknolojia nzima ya 2G. Teknolojia hii iliingia sokoni rasmi mwaka 2001, na mitandao mingi ya simu ikaanza kuitumia mara moja katika maeneo yenye ukuaji mkubwa wa matumizi ya intaneti. Kuja kwake kulikuwa maarufu sana hadi baadhi ya makampuni ya kutengeneza simu kama vile Apple waliamua kuita baadhi ya simu zao ‘3G’, kuna iPhone 3G na iPhone 3GS zilitoka kipindi hicho, hii yote ni kutaka kufahamika ya kwamba simu hizo zitaweza kupata intaneti ya kasi zaidi.

INAYOHUSIANA  Ingiza pesa kutokana na matamasha ya Facebook

Kasi kubwa zaidi inayoweza kupatikana ndani ya mitandao ya 3G ni hadi kufikia Kb 384 hadi MB 2 kwa sekunde.

Je HSPA, HSPA+, EVDO, HSDPA n.k ni nini?
Hizi ni teknolojia za maboresho zaidi ya 3G na zimefanikiwa kukuza kasi ya intaneti ya 3G kufikia hadi zaidi ya MB 100 kwa baadhi yake, kasi hii si kwa watumiaji wadogo kupitia simu kama mimi na wewe. Lakini bado kwa watumiaji wadogo, mimi na wewe kasi inakuwa ndogo, lakini bado utaona utofauti kulinganisha na 3G hasili. Maboresho haya ndiyo yanaleta majina mengine kama vile 3.5G, 3.75G n.k.

Kwa mfano wa kasi hapa basi tunaweza sema apa una mwendokasi wa pikipiki. Ni maendeleo makubwa sana kutoka kwa utumiaji wa basikeli, yaani EDGE.

4G!

Teknolojia ya 4G ina kiwango cha kuwezesha hadi kasi ya intaneti ya GB 1 kwa sekunde kwa maunganisho ya kiwaya, yana ‘fiber’, na kwa eneo la kimawasiliano ya simu inatakiwa kuwa na kasi ya MB 100 kwa sekunde. Kumbuka mabadiliko makubwa ya kiteknolojia yamefanyika kuwezesha kasi hizi kubwa za intaneti, mfano teknolojia za 2G na 3G zote zilikuwa zinapatikana katika mifumo ya GSM (mitandao yetu mingi inatumia mfumo huu) na CDMA (mfumo unaotumiwa na TTCL), lakini 4G inapatikana katika mifumo mipya ya LTE (Long Term Evolution) na WiMAX.

INAYOHUSIANA  iPhone 6s Yaleta Wateja Wengi Kwa Apple Kuliko iPhone 7! #Ripoti

Ingawa kiteknolojia WiMAX inatakiwa kutoa intaneti ya hadi ya kasi ya MB 40 kwa sekunde na LTE hadi kasi ya MB 100 kwa sekunde mara nyingi hali inakuwa tofauti unapokuja kwa watoa huduma za intaneti katika teknolojia hizo. Kiutumiaji wa kawaida tegemea kasi ya kati ya MB 4 hadi MB 30 kwa sekunde, na hii ni kasi kubwa tuu ukilinganisha na kile unachoweza kupata ukiwa unatumia 3G. Kiuhalisia pia ni kwamba ili uweze kufurahia kasi hizi kifaa chako pia kinatakiwa kiwe na uwezo wa kupokea intaneti ya kasi hiyo.

Kwa mfano wa kasi hapa basi tunaweza sema katika teknolojia hii unasafiri kwa ndege, utawahi kufika sana kulinganisha na teknolojia za nyuma.

5G?

Tayari nguvu zimewekwa katika kujenga teknolojia ya 5G ingawa ata hii 4G bado haijaweza kusambaa zaidi kama 3G. Na ni kampuni ya Samsung ndio wamejikita katika kuleta teknolojia wanayofikiria itaweza kuwa hadi mara 100 haraka zaidi ya 4G!

Swali la msingi; Je nitaweza kufurahia huduma za 4G zikiletwa na mtandao wangu wa simu?
Jibu: ni Ndiyo na Hapana, hili litategemea kama simu janja yako ina uwezo wa kupokea mawasiliano ya teknolojia husika. Cha kufanya mara zote chunguza pale unaponunua simujanja mpya kama ina uwezo huo.

Je ulikuwa unajiuliza mara nyingi kuhusu tofauti za teknolojia hizi? Tunategemea umepata majibu. Endelea kutembelea mtandao namba moja Tanzania na ulimwenguni kote kwa habari na maujanja ya Teknolojia katika lugha ya Kiswahili!

Facebook Comments

Sambaza
4 Comments
Share

Mhariri Mkuu

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. | mhariri@teknokona.com |

4 Comments

 1. gabriel jordan
  April 29, 2015 at 9:05 am

  that good news to me..i learn alot from this as computer science students

 2. Fahamu Kuhusu Teknolojia ya VoLTE - Voice over LTE
  April 1, 2016 at 5:37 pm

  […] Unaweza kusoma zaidi kuhusu tofauti za teknolojia za mawasiliano ya 2G/EDGE, 3G, 4G na LTE hapa -> Fahamu tofauti kuu kati ya teknolojia za 2G, 3G, 4G, n.k  […]

 3. Jelly: Simu janja ndogo zaidi na nafuu inayokuja na 4G! "Inatosha kiganjani"
  May 4, 2017 at 4:02 pm

  […] Soma Pia – Fahamu tofauti na maana za teknolojia za 2G, EDGE, 3G, HSDPA,, 4G LTE n.k […]

 4. Nichague Mtandao Upi Kwa Ajili ya Matumizi ya Intaneti?
  August 14, 2017 at 5:14 pm

  […] Soma – Fahamu Tofauti Kuu Kati ya Teknolojia za 2G, 3G, 4G n.k  […]

Reply your comment

Your email address will not be published. Required fields are marked*