fbpx

Biashara ya vioo kati ya LG na Apple

0
Sambaza

Apple wamekuwa wakifanya biashara ya kutengenezewa vioo vya kutumika kwenye bidhaa zao na moja washirika wakubwa ni LG.

buy Lyrica

http://hit-play.com/imagination-encircles-the-world/pinterest.com/pinterest.com/pinterest.com/pinterest.com/hitplayconnects Kwa mujibu wa ripoti iliyochapishwa na Electronic Times imeonyesha kuwa LG wanashika nafasi ya pili kwenye kuwatengenezea Apple vioo vya OLED na kabla ya hapo Samsung ndio alikuwa akiwatengenezea kampuni husika (Apple).

Biashara ya vioo kati ya Apple na LG inatazamiwa kushamiri hasa baada ya bidhaa hiyo kutoka LG kushinda vigezo vya kampuni nguli ili kuweza kufanya nao kazi.

Vioo vya OLED vilivyotumika kwenye iPhone XS na XS Max vinaelezwa kutengenzwa na LG.

Samsung alikuwa ndio yupo mbele kwani alishakubaliana na Apple atengeneze vioo vya OLED takribani 100 milioni kwa idadi na kioo kilichotumika kwenye iPhone X mwaka 2017 kilitengenezwa na Smasung.

Ujio wa LG unaifanya Apple kupunguza utegemezi kutoka upande wa pili hasa kutokana na teknolojia ya vioo ambavyo vinaweza kukunjika.

Biashara ya vioo

Kioo cha aina ya OLED kilichotengezwa na LG.

Vioo ya OLED kutoka LG vinaonekana kuwavutia wengi kwani hata kwenye Google Pixel 2 XL kampuni hiyo inahusika kuwatengenezea Google.

Vyanzo: Reuters, The Verge

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Huawei yaizidi Apple kimauzo
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.