fbpx

BoomPlay Music Yashinda Tunzo Ya App Bora Afrika! #AppsAfrica

0
Sambaza

BoomPlay ni jukwaa kubwa la mtandaoni ambalo linakusadia kupakua na kusikiliza miziki na kutazama video kutoka kwa wasanii wako pendwa.

Mchango wa BoomPlay  bila shaka umeonekana na hii imipelekea kunyakua tunzo kama App bora kutoka Afrika. Tunzo hizi zinatolewa na Apps Africa, ambayo ni  tovuti inayojihusisha na habari za kitekinolojia na utoaji wa ushauri wa kitaalamu unaoangazia ufahamu wa maswala ya simu, tekinolojia na ubunifu.

App ya Boomplay Music inakuwezesha kupata nyimbo zaidi ya milioni , video za kutosha na  habari kede kede za burudani. 

App inaongeza watumiaji wake kila siku kutokana na huduma bora wanayoitoa. Mpaka kufikia mwezi Oktoba mwaka huu tayari App ilikua na watumiaji milioni 15, wakati kwa mwaka 2016 mwishoni walikuwepo watumiaji milioni 6 tuu.

INAYOHUSIANA  Google Hangouts kufikia tamati ya kutumika

Timu Ya BoomPlay Music

Unaweza ukashangaa kwa nini idadi ya watumiaji inaongezeka?

Jibu ni kwamba, urahisi wakuitumia, mwonekano mzuri na ubunifu, haswa kwa namna inavyorahisisha upatikanaji wa muziki  kwa mamilioni ya waafrika, na kuchochea wanunuzi wa muziki kuongezeka, wakati ikisaidia kupunguza uharamia kupitia mikakati mizuri ya kibiashara, kuhakikisha hati miliki zinalindwa kwa jitihada zote na pia  hizi ndio sababu zilizofanya App ya BoomPlay Kushinda tunzo hiyo.

BoomPlay ilishindanishwa na App nyingi, zikiwemo Carter – Afrika kusini, Asorbia – Ghana, Truecaller Africa and FeastFox – Afrika Kusini. Mwisho wa siku ilitoka kidedea na kuwabwaga mbali wawaniaji wengine na kuwa App ya kwanza ya kupakua na kusikiliza muziki kushinda tuzo hiyo.

Wakati wanakabidhiwa Tunzo hiyo huko Afrika kusini, Mkurugenzi mkuu Bw.  http://thomsenoilco.com/?p=85 Joe He alisema enter site :  “Kunyakua tuzo ya  Best African App kunaonyesha kufanikiwa kwa jitihada zetu za kujenga mfumo bora na endelevu kwa wamiliki wa kazi za sanaa ya muziki, wakati huo huo tukihakikisha kazi za sanaa ya muziki zinawafikia watumiaji kwa urahisi zaidi.  Kwa kipindi kifupi tu cha miaka miwili mafanikio tuliyoyapata ni ya kuvutia”.

Kampuni inaamini kwamba wamiliki wa kazi za sanaa ya muziki  wanaweza kufaidika na mauzo ya kazi zao. Zaidi ya watumiaji milioni 2 kwa sasa wanatumia app kusikiliza muziki, kutazama video na kusoma habari kila siku.  

BoomPlay Kwa  Android ingia hapa kuipakua

INAYOHUSIANA  Google Playstore ina muonekano mpya

BoomPlay Kwa iOS ni mpaka 2018

TeknoKona inatoa pongezi sana kwa App ya BoomPlay Kwa kunyakua tuzo hii ya ubunifu (AppsAfrica Innovation 2017) kwa bara la Afrika.

Ningependa kusikia kutoka kwako, wewe habari hii unaipokeaje? Toa neno la pongezi kwa BoomPlay. Niandikie hapo chini sehemu ya comment.

Kumbuka Kutembelea TeknoKona Kila Siku Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa Teknokona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comments are closed.