fbpx
Kompyuta, Maujanja

EaseUS Data Recovery Wizard: Programu ya Kufufua Mafaili Yaliyokwishafutwa

easeus-data-recovery-programu-ya-kufufua-mafaili-yaliyokwishafutwa
Sambaza

EaseUS Data Recovery ni programu ya bure inayokusaidia kutafuta, na kuchagua kurudisha hai mafaili uliyokwisha yapoteza kwa njia kama vile kufuta bahati mbaya, kuformat diski zako (HDD, USB Flash Drive) n.k.

Easeus Data Recovery Wizard

Tulishaandika kabla makala kuhusu – Jinsi Ya Kufufua Mafaili Yaliyofutwa Katika Simu au Kompyuta  katika makala hiyo tuligusua zaidi programu kutoka kampuni ya Asoftech na muda huu tunaangalia jinsi ya kufanikisha jambo hilo hilo kupitia programu ya kisasa zaidi ya EaseUS Data Recovery kutoka kampuni ya EaseUS.

  • Asoftech Data Recovery kama uliijaribu ilikuwa inakupa uwezo wa kujaribu tuu – zaidi ya hapo lazima ulipie. Kwa EaseUS Data Recovery ni bure kuokoa (recover) data hadi GB 2 Bure.

ease data recovery

Sifa zake;

Programu hii inaweza kuokoa aina zote za mafaili yaliyopotea, hii ikiwa ni pamoja na picha, document, video, mafaili ya sauti (nyimbo, n.k), na mafaili ya aina nyingi.

Kupitia programu hiyo unaweza okoa mafaili kutoka kompyuta, laptop, ‘hard drive’ – (SSD, HADD, USB nk), na vifaa vingine kama vile simu na tableti pale unapoziunganisha na kompyuta yenye Ease US Data Recovery.

Iwe faili limefutwa bahati mbaya, limefichwa, au kupotea kwa aina yeyote katika diski yako. Utaweza kuiokoa.

Idadi nzima ya mjumuisho wa ukubwa wa data unazoweza ku’recover hauna kikomo ila kwa toleo la bure unaweza kurudisha hai mafaili ya hadi GB 2. Hii ni tofauti na programu tuliyoiangalia mwanzo, ya Asfotech ambayo uwezi kurudisha hai mafaili yeyote bila kulipia.

INAYOHUSIANA  Kompyuta/Tabiti isiyochosha kuibeba

Ukifungua programu mara ya kwanza utaona umeambiwa kuna 500MB za bure kuokoa, ila kwa kitendo cha kushare kwenye mitandao ya kijamii moja kwa moja kutoka programu hiyo unapata GB 1.5 ya zaidi.

Utumiaji

  • Ukishapakua na kufungua programu hii mara ya kwanza utaona sehemu inayokupa nafasi ya kuchagua aina ya mafaili unayotaka kuyarudisha hai (recover). Pia utaweza kuchagua ni diski (drive) gani unataka kuokoa data zako, kama ni diski ya USB (Flash Drive, HDD n.k).
  • Baada ya hapo utapata matokeo na utaweza kuchagua mafaili unayoitaji ku’recover.
INAYOHUSIANA  Simu ipo slow?? Fanya yafuatayo irudie kasi yake! #Maujanja

Je umekwishatumia programu yeyote kwa ajili ya kuokoa mafaili uliyokwisha yafuta (delete/format)? Tuambie ulitumia programu gani kufanikisha kupata data zako?

Pakua/Download – http://www.easeus.com/data-recovery-software/

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Mhariri Mkuu

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. | mhariri@teknokona.com |